MABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet leo mapema wamefanikiwa kufika katika eneo la Mwenge jiji Da-es-salaam na kutoa msaada kwenye Zahanati inayopatika eneo hilo ikifahamika kama Mlalakuwa.

Huu ni utaratibu ambao Meridianbet imekua miaka na miaka wa kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yake, Ndivyo walivyofanya leo baada kufika kwenye Zahanati ya Mlalakuwa na kutoa msaada wa vifaa vya kuhifadhia takataka (Dustbins) ili kuimarisha usafi kwenye Zahanati hiyo.

Meridianbet wamefanya hivo kwakua hospitali ni sehemu ambayo inatoa huduma za kiafya hivo itakua sio jambo la busara kama sehemu ya kutoa huduma za kiafya ikawa sehemu ya kuharibu afya kwasababu ya uchafu, Na ndio maana mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wameamua kutoa msaada wa vifaa vya kuhifadhi takataka.

Aidha mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi. Nancy Ingram alipata wasaa wa kuongea baada ya kutoa msaada wa vifaa hivo "Meridianbet tunajua na tunathamini sana umuhimu wa Utunzaji wa Mazingira hasa hasa katika zahanati, Kama wadau wa utunzaji wa mazingira tutaendelea kuimarisha na kuhamasisha zaidi utunzaji wa mazingira."

"Pia tunashukuru Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa na Uongozi wa Zahanati ya Mlalakuwa kuungana na sisi katika zoezi hili nakutuunga mkono katika hili tulilolifanya leo”

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye ligi mbalimbali barani ulaya na dunia kwa ujumla. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Mganga Mfawidhi katika Zahanati hiyo ya Mlalakuwa inayopatikana maeneo ya Mwenge Bi. Zamzam Said Omar alipata nafasi ya kuzungumza na kutoa shukrani zake kwa Meridianbet “Kiukweli ningependa kuwashukuru sana Meridianbet kutuchagua sisi Zahanati ya Mlalakuwa kua moja ya Zahanati ambazo zimepata msaada huu, Lakini kubwa zaidi ni sisi tutahakikisha tunaimarisha usafi eneo hili kwani kwa msaada huu mmetupa sisi deni asanteni sana”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...