Na Mwandishi Wetu

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo, amezitaka kampuni za usafiri mtandaoni kuajiri vijana wenye sifa ya kudadisi abiria wanaowabeba kwa maswali yenye mwelekeo wa kutambua masuala ya usalama.

Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya taxi mtandaoni maarufu kama SUKA.

Murilo alisema kampuni zinazotoa huduma za usafiri mtandaoni ni mdau muhimu sana kwa serikali kwa masuala yanayohusu usalama kwani wanahudumia watu wengi tofauti.

“Unapoingia kwenye kutoa huduma kama hii automatically wewe ni wakala wa serikali lazima uwe mdadidi siyo kwa maswali yenye maudhi lakini maswali yenye mwelekeo wa kutambua masuala ya usalama,” alisema

Alisema kuna Kampuni zilizokuwa zinatoa huduma zinazofanana na SUKA hivyo kuwataka wamiliki wa kampuni hiyo kufuatilia kujua walifanikiwa kwa kiwango gani na walikwama wapi wakati wa kufanya shughuli zao.

“Fuatilieni mjue kumbukumbu za kampuni hizo zikoje kwenye mamlaka zilizofanya usajili wake na wananchi ambao walikuwa wanapata huduma hizo wanazungumziaje kampuni hizo ili mpate mwelekeo sahihi wa kazi zenu,” alisema.

Murilo alisema anaamini wamiliki wa kampuni ya SUKA wamefanya utafiti na kuamua kuingia kwenye utoaji wa huduma hiyo wakiwa na malengo makubwa ya kuboresha zaidi huduma hiyo kuhakikisha hakuna malalamiko ya wateja.

Kamanda Murilo alisema miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikilalamikiwa na wateja kwenye kampuni zilizokuwa zinatoa huduma kama hiyo ni tabia zisizo ridhisha za watu waliokuwa wakiendesha vyombo vya usafiri.

“Tabia zile zilishusha heshima ya huduma hiyo na watu walikuwa wakipata mrejesho wa lugha wanazopata kutoka kwa wahudumu wale , tabia ni pamoja na uvaaji ukihudumia watu lazima uvae mavazi ya heshima,” alisema

Aliwataka kutoa mafunzo ya mara kwa mara ya namna ya kutoa huduma hiyo ili kuhakikisha watoa huduma wanakuwa waadilifu kwa wateja na kuondoa malalamiko.

Naye Ofisa Mawasiliano wa SUKA , Luciana Mwambinga, alisema waliamua kuanzisha huduma hiyo baada ya kuona heka heka za maisha ya kila siku na mahitaji ya usafiri hasa kwa watu wasio na magari kwa kutengeneza daraja linalofanikisha mawasiliano kati ya watoa huduma na watumiaji kwa urahisi.

Alisema SUKA ni mfumo bora unaowaunganisha abiria na madereva kwa urahisi, ufanisi, usalama zaidi na kwa gharama nafuu ambapo wameboresha zoezi zima la upatikanaji wa usafiri kupitia mtandao kati ya abiria na watoa huduma ya usafiri.

“Tunatambua kuwa abiria na dereva wote wanahitaji mazingira bora yenye ufanisi na usalama ili waweze kufanya shughuli zao vyema na kwa kuzingatia hayo SUKA imelenga na inapatikana kwa watumiaji wote wa usafiri na tembelea www.sukaride.com upate taarifa zaidi,” alisema

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya usafiri mtandaoni maarufu kama SUKA leo jijini Dar es salaam. 

Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alex Katundu akizungumza nkwenye uzinduzi huo wa taxi mtandaoni  inayojulikana kwa jina la  SUKA

 

Afisa Leseni na Usajili wa LATRA, Jonathani Kitururu  akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...