Asasi isiyo ya kiserikali ya Ndalini Media Solution imezindua makala maalumu ya kupambana na matumizi ya mkaa na kuni ili kupunguza athari za mabadiliko ya Hali ya hewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua makala hiyo mkurugenzi wa tasisi hiyo Anna Masawe amesema dhumuni la kuu la Kuja na makala hiyo ni kufunga mkono juhudi za Rais mama Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati salama ili kulinda mazingira ya Taifa letu.

Bi Masawe ameongeza kuwa Bado Kuna kazi kubwa inahitajika ili kuishawishi jamii hasa iliyopo maeneo ya vijijini kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni na kuanza kutumia nishati mbadala ikiwemo gezi na umeme.

Mbali na hayo Bi Masawe ameiomba serikali kupitia upya Bei za nishati mbadala ili wananchi wa kawaida waweze kumudu Gharama za nishati hizo ili kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.

Kwa upande wake Fred Mwilinda kutoka balaza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira amesema elimu inahitajika zaidi kuelimisha jamii madhara ya matumizi ya nishati chafuzi na amewataka wadau ikiwemo vyombo wa habari kutumia nafasi zao kutoa elimu sahihi ya mazingira kulinda mazingira ili jamii iweze kuhama na kuondokana na matumizi ya nishati chafuzi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...