Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetambulisha Rasmi mpango wa uchangiaji wa hiari ulioboreshwa kwa Wadau wa Sekta isiyo Rasmi Mkoani Kagera katika Kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Jengo la Mafao Mkoani humo Machi 18, 2024.

Akitoa hotuba yake katika Utambulisho wa Mpango huo, Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema kuwa Serikali inao wajibu wa kuweka mazingira ya Kisera na Kisheria kwa lengo la kuhakikisha pamoja na mambo mengine, kila Mwananchi anapata Kinga wakati wa Uzee, ugonjwa na Ulemavu, ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 11 ibara ndogo ya kwanza.

Akiongea kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Bwn. Large Materu Meneja wa NSSF Kinondoni ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF amesema kuwa lengo la Mpango huu ni kuhudumia Vikundi vya Kijamii vilivyosahaulika lakini vimekuwa na Mchango mkubwa katika Uchumi wa Nchi, kwa kuvifikia na kuviingiza katika Mpango wa uchangiaji, ikiwa ni sambamba na kuunga kwa vitendo kauli ya Serikali ya kupunguza Ufukara na Umaskini katika Jamii na kuchochea Kasi ya Maendeleo na Uchumi katika Taifa letu

Aidha Bwana Materu amesema mpango huu kwa mara ya kwanza utampa Mwanachama Mjasiliamali wa Kawaida kupata Fao la matibabu, pensheni, uzazi,  Fao la kujitoa, na Fao la Mazishi ikiwa atafariki akiwa Mwanachama, zote zikiwa ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Kwa upande wake Meneja wa NSSF Mkoa Kagera Bwn. Siraji Kisaka, amesema kuwa awali kupitia Mpango huo wa uchangiaji wa hiari awali  Wanachama hawakuweza kupata huduma ya Matibabu, lakini pia haikuwezekana kutoa kiasi cha Pesa kwa ajili ya kutatua changamoto na kuendelea na uanachama, na haikuwa rahisi kwa Mwanachama kujichangia, na kuongeza kuwa kabla ya Mabadiliko ya Sheria ya Mwaka 2018, Kundi la wavuvi wakulima, mama Lishe, bodaboda na Wajasiliamali Sheria ilikuwa haiwatambui kufikiwa na kupatiwa huduma ya  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. kumfuata, lakini kwa Sheria hiyo inautaka mfuko kuwafikia Wananchi katika makundi hayo yote na kuwapatia  Elimu ya mpango huo.

Sambamba na hilo Maboresho mengine yaliyofanyika katika Mpango huo ni pamoja na Mwanachama kuwa Uwezo wa kujichangia mwenyewe kupitia mifumo ya simu za mkononi, kupitia mabenki na hata kwa Mawakala wa huduma ya kifedha,  Uwezeshaji wa kujichangia Fedha kidogo-kidogo kwa kudunduliza kulingana na kipato cha Mwanachama, Uwezeshaji wa kuchangia kwa kurudi hadi Miezi 12 nyuma pale ambapo Mwanachama amepata upungufu wa kipato cha uchangiaji.

Maboresho mengine ni pamoja na Kumpa fursa Mwanachama kupunguza akiba yake Ili iweze kumsaidia kutatua changamoto za dharura katika kipindi husika, Kumuwezesha Mwanachama kuchangia kwa kurudi hadi Miezi 12 nyuma pale ambapo amepata upungufu wa kipato cha uchangiaji, na pia Mwanachama atakuwa na uwezo wa kuchukua Michango yake yote pindi atakapohitaji kusitisha Uanachama wake kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi au Kijamii na mengine mengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...