Na.Vero Ignatus,Arusha

Kikao cha kwanza cha Tathmini sekta ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Kati ya Wizara ya Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari na wadau wa sekta ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari kimefanyika machi 18,2024 Jijini Arusha kikiwa na lengo la kuandaa utaratibu uliobora wenye Tija kwa Taifa

Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao hicho Waziri wa Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye, amesema Malengo ya Wizara hiyo ni kuwa na jamii inayofikiwa na Habari sahihi utoaji wa huduma za uhakika kwa kuweka mazingira yanayojenga ubunifu kwa kuiwezesha Tanzania kukua kiuchumi.

Waziri Nape amesema kuwa kikao hicho kimeweza kuwa na washiriki 200 na wengine 3000 wakifuatilia kwa njia ya mitandao,amesema wizara yake iko katika utekelezaji wa Falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan inayotaka kuvibeba vyombo vya habari kwa tija na maendeleo ya Taifa.

Amesema, kupitia Falsafa hiyo, yako mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika usimamizi wa vyombo vya habari ikiwemo kuepuka kuchapana viboko vya faini na kufungiana, alisema, sio kwamba makosa hayapo bali wanatumia busara katika kufumbia macho kasoro ndogondogo zinazojitokeza huku wakiwashauri wahusika kurudi katika mstari wa maadili ya vyombo vyao vya habari.

"Sekta ya utangazaji zamani mkiandikiwa barua mnaandaa faini kabla ya kwenda, leo mkiona barua mnakimbia na mnaenda kupewa kahawa na juice na kushauriwa. Habari maelezo sijasikia kesi siku nyingi wala kusikia gazeti limefungiwa, hiyo ni mageuzi makubwa yamefanyika kwenye namna tunavyoshughulika na sekta yetu” alisema Waziri Nape.

"Tunahitaji kweli kwenda pamoja na imejithibitisha kwa mda mfupi kuwa, kumbe viboko na kuchapana sio njia pekee inayoweza kutufanya tusonge mbele bali hata tukikaa na kuridhiana inawezekana kwani mafaini yasiyo na kichwa wala miguu wakati mwingine yanakwaza uwekezaji”

Katibu mkuu Wizara ya habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla amesema kuwa, Serikali kupitia Wizara hiyo imeendelea kutekeleza majulumu yake ya Misingi ikiwa ni pamoja na mapitio ya sera ya Haifa ya tehamanya mwaka 2016,ambapo Wizara iimekamilisha rasmi sera ya Taifa ya Tehama ya 2024 ambayo ipo hatua ya kuridhiwa

" Sera hii inakwenda kuweka mwelekeo wa Taifa katika masuala ya Tehama kwa sekta ya umma na sekta binafsi, shambamba na majukumu ya Tume ya Tehama nchini.

Aidha Wizara imendelea na ujenzi wa mkongo wa Taifa kwa zaidi ya kilometa 3000 mbao utawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu, vile vile serikali imeingia mkataba na watoa huduma za mawasiliano nchini kwaajili ya ujenzi wa minara 758 katika kata 713 pamoja na kuongeza nguvu minara 304 kutoka 2G na kukamilisha anwani za makaziPamoja na kukamilisha tathmini ya awali ya Hali ya kimazingira na jamii katika maeneo 136 yatakayojengwa minara mipya

"Wizara imeweka mango wa magunzo ya mida mrefubna mfupi kwa watumishi wa umma 500 kwaajili ya kuongeza ujuzi kwenue manual ya Tehama, Kati ya watumishi hao 15 ni Maprofesa kutoka chuo Kikuu Dar es salaam, Chip Kikuyu Dodoma ,Chuo kikuu cha Mbeya cha Sayansi na teknolojia (MUST) , watakwenda kusoma magunzo ya mida mrefu kwa eneo la teknolojia zinazoibuka"

Vilevile Wizara inaendelea na ujenzi wa vituo vya kuhifadhia taarifa (Data Centre)Zanzibar na Dodoma,vituo vya kutolea huduma pamoja 32 vinatarajiwa kujengwa kwenye makao makuu ya kila mkoa Tanzania bara na Zanzibar, inatarajia kutekeleza mradi wa maghala ya kuhifadhi bidhaa zinazouzwa au kununuliwa kwa njia ya mtandao.

" Wizara kupitia Tume ya TEHAMA inatekeleza mradi wa kujenga Vituo vya Ubunifu 8 I like kuwezesha vijana wajasiriamali kutekeleza masuala ya ubunifu"Alisema Katibu

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Mussa Juma ameiomba Wizara kuangalia maslahi ya waandishi haswa katila mikataba na ajira kwani 80% ya waandishi wa habari hawajaajiriwa

Aidha mwenyekiti huyo ameiomba pia serikali kushirikiana na wadau mbalimbali kutengeneza muongozo kwaajili ya ulinzi na Usalama kwa Waandishi wakati wa uchaguzi.
Waziri wa Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye, akizungumza katika Kikao cha kwanza cha Tathmini sekta ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Kati ya Wizara ya Habari mawasiliano na Teknolojia ya Habari na wadau wa sekta binafsi
Katibu mkuu Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla, akifuatilia kwa makini kile kinachoendela
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, (TCRA) Rolf Kibaja katika kikao cha Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kinachofanyika 18 Machi, 2024 jijini Arusha
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi. Justina Mashiba akitoa taarifa ya utendaji wa Mfuko huo wakati wa kikao cha Tathmini ya Utendaji wa Serikali na Sekta Binafsi katika Sekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA kilichoandaliwa na Wizara ya Habari,

Baadhi ya Viongozi, Wakurugenzi, na Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakifuatilia kikao cha Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kinachofanyika leo tarehe 18 Machi, 2024 jijini Arusha

Baadhi ya Viongozi, Wakurugenzi, na Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakifuatilia kikao cha Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kinachofanyika leo tarehe 18 Machi, 2024 jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...