Na Mwandishi Wetu,Tanga

JESHI la Polisi Wilaya ya Tanga limetoa shukrani kwa Ubalozi wa Uswisi nchini kwa kuwezesha mradi wa mafunzo ya elimu ya usalama barabara kwa madereva bodaboda wa Jiji la Tanga kwani utasaidia kuondoa changamoto za makosa ya usalama wa barabara.

Shukrani hizo zimetolewa na Mkuu wa usalama wa barabara wilayani  Tanga Abel Kigai alipokuwa akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayotekelezwa na Amend Tanzania kwa ufadhili wa Uswisi ambapo ameeleza mafunzo yatasaidia kupunguza ajili za barabarani katika Jiji hilo.

Amefafanua kwamba kumekuwa na changamoto ya makosa ya barabara yanayofanywa na madereva wa bodaboda ambayo wakati mwingine yanasababisha uvunjifu wa amani ni inatokana na kukosa uwelewa wa sheria.

Ameongeza kuwa kupitia  mafunzo hayo wamefundisha elimu ya kuwataka wajiepushe na makosa ya kujichukulia sheria mkononi pale ambapo wanapopata ajali kwa kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kujieupusha na vitendo vya uhalifu inapotokea ajali.

Kwa upande wake Ofisa Miradi Mwandamizi Mratibu  kutoka Taasisi ya Amend Ramadhani Nyaza amesema kwamba mpaka sasa wamekwenda madereva bodaboda 180 wakiwa na lengo la kufikia madereva 500.

"Mradi huu ambao unafadhiliwa na ubalozi wa Uswizi unalengo la kuwafikia vijana 750 wanaofanya shughuli za usafirishaji kwa kutumia bodaboda katika mikoa ya Tanga na Dodoma"amesema Nyanza.

Wakati huo huo Diwani wa Kata ya  Mabawa Athumani Babu amesema kwamba  mradi huo wa elimu utapunguza  changamoto ya ajali za barabara kwenye maeneo mbalimbali Jiji Tanga ambapo amesisitiza mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa.

Hata hivyo madereva wa bodaboda waliopatiwa mafunzo walisema kuwa wataweza kuwakuwa mabalozi Wazuri wa kuendeleleza elimu hiyo Kwa wenzao Ili kupunguza changamoto ya uwepo wa ajali za barabara.

"Tunakwenda kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani kupitia shughuli zetu za bodaboda lakini na kuwashawishi wenzetu wengine kuachana na tabia za kujichukulia sheria mkononi lakini na kufuata sheria za usalama barabara "amesema dereva bodaboda Nasib Issa











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...