Na Janeth Raphael - MichuziTv -Bungeni Dodoma

Serikali imependekeza bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 49,345.7 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi bilioni 44,388.1.

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amewasilisha mapendekezo haya kwenye Kamati ya Bunge zima leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma,

Kati ya mapato hayo, mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa shilingi bilioni 29,858.4, mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea shilingi bilioni 3,408.1; na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi bilioni 1,344.1.
19.

Dkt Mwigulu amesema makadirio ya mapato kwa mwaka 2024/25
yamezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo mwenendo halisi wa ukusanyaji wa
mapato; mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla; na jitihada zinazoendelea
kuchukuliwa na Serikali katika kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.

"Sehemu kubwa ya bajeti (asilimia 70.1) itagharamiwa na mapato ya ndani ambayo yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 10.0 mwaka 2024/25."

Serikali itaendelea kuweka msukumo na jitihada za kuimarisha ukusanyaji wa
mapato ya ndani kwa kuwa ndicho chanzo chenye uhakika na kisicho na masharti hasi katika kugharamia bajeti ya Serikali. 

Aidha ongezeko la mapato ya ndani limetokana na
hatua mbalimbali za kiutawala na kisera zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti ya Chama cha Mapinduzi katika kusimamia ukusanyaji wa mapato

Dkt Mwigulu amesema hatua hizo zinajumuisha: uanzishaji wa Tuzo ya
Uzalendo ambayo maandalizi yake yapo katika hatua za mwisho; uboreshaji wa
mifumo ya TEHAMA, ikiwemo mfumo wa uthaminishaji wa mizigo wa forodha
(TANCIS) ambao utafungamanishwa na mfumo wa kodi za ndani (IDRAS);
kupunguza matumizi ya fedha taslimu katika uchumi (less cash) ikiwemo matumizi ya mfumo wa malipo ya kielektroniki (Tanzania Instant Payment System) utakaopunguza gharama za miamala; kuendelea kuwekeza katika sekta za uzalishaji na maeneo yenye matokeo ya haraka (quick wins) ili kuongeza wigo wa kodi; kuendelea na hatua za urasimishaji wa sekta isiyo rasmi; kutoa elimu ya mlipakodi kwa umma ili kuongeza uhiari wa kulipa kodi; na kuendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi ikijumuisha uboreshaji wa vituo vya utoaji huduma kwa
pamoja mipakani (OSBP).

Aidha, Serikali inakamilisha uandaaji wa Mkakati wa muda wa Kati wa Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani utakaoainisha hatua mbalimbali za kuongeza mapato ya ndani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...