Morogoro 12 Marchi 2024 T-MARC Tanzania kwa kushirikiana na Strength Inspiration,liliadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kushiriki mazungumzo na vijana 40 mkoa wa Morogoro, kata ya Chamwino ikiwa ni kelele cha kusherekea siku hiyo muhimu kwa wanawake. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Afisa Maendeleo wa Kata ya Chamwino na yalienda sa kauli mbiu ya mwaka huu "Wekeza kwa Wanawake, kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii.”
Mazungumzo hayo yaliangazia uzoefu wa vijana wanaoshiriki katika mradi wa Kijana Nahodha. Washiriki walishiriki waziwazi safari yao na jinsi mradi huo umenufaisha maisha yao kwa njia chanya. Mmoja wao alielezea kuwa kwa sasa ameweza kufanya biashara ndogo ndogo na kumlea mtoto wake. Badilishano hili  lilihimiza vijana kushirikiana pamoja.
Akizungumza mara baada ya sherehe hizo, Mwakilishi wa T-MARC Tanzania Toyi Dadi alisema kuwa T-MARC Tanzania inatambua changamoto zinazokabiliwa na vijana na na hivyo ni muhimu kutoa suluhu zinazowezekana na mifumo ya usaidizi iliyopo kupitia T-MARC Tanzania na Strength Inspiration huku akiweka mkazo kwa Vijana kushirikiana pamoja na kufanya kazi pamoja ili kujenga mtandao wenye nguvu zaidi na kutetea mahitaji yao.
‘Kwa kujenga jukwaa la vijana kushiriki uzoefu wao na kupata rasilimali muhimu, mazungumzo haya ya jamii yanaashiria dhamira ya Siku ya Wanawake Duniani.  Nguvu ya Wanawake na kujitolea kwa T-MARC kwa kuwawezesha mama vijana kunufaisha njia ya mustakabali mzuri, sio tu kwao bali pia kwa watoto wao na jamii kwa ujumla’.
Kilele cha Sherehe za kuadhimisha za Siku ya Wanawake Duniani zilifanyika Ijumaa ya 8 Machi 2024 kwenyeViwanja vya Mkambarani, Wilaya ya Morogoro kwa kuandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo T-MARC na Strength Inspiration na kuongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Joanfaith Kataraia,
Sherehe hizo zilijuimusha burudani mbalimbali kama vile ngoma, muziki pamoja michezo mbali mbali huku pia wanawake wakipata fursa ya kuonyesha bidhaa zao walizozitengeneza. Na kuonyesha kushukurani kwa wanawake katika kuleta maendeleo kwenye jamii, T-MARC Tanzania walitoa box 30 za pampers pamoja na box 4 za taulo za kike.
Maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani pia yalitoa fursa kwa wanawake kuungana pamoja, kusherehekea mafanikio yao, na kujadili changamoto wanazokabiliana nazo huku mashirika ya T-MARC na Strength Inspiration yakionyesha mchango wao katika kuwawezesha wanawake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...