Na Rahma Khamis Maelezo. 12/3/2024

Serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imewataka wananchi kuacha kula nyama ya kasa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kifo.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofisini kwake Mnazimmoja Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe Hassan Khamis Hafidh amesema hatua hiyo imekuja kufuatia vifo vya watu tisa na wengine 18 kulazwa katika Hospitali ya Abdalah Mzee kati ya watu 160 waliokula nyama hiyo inayosadikiwa kuwa na sumu.


“ watu tisa wamefariki kutokana na kula nyama hiyo na zaidi ya watu 15 kulazwa katika Hospitali Abdallah Mzee ” Alifahamisha naibu waziri


Aidha Wizara inatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba na waliopata madhara na kuwataka wananchi kuacha kabisa kula nyama ya kasa ili kuepuka madhara yatokananyo na nyama hiyo.


"Kutokana na Utafiti uliyofanywa kitaalamu na kubainika kuwa na nyama hiyo kua na sumu na kupelekea kifo" alifahamisha.


Akitoa taarifa ya kitaalam Mkemia Mkuu wa Serikali Faridi Mzee Mpatani amesema kitaalamu kuna aina saba za kasa ambapo katika aina hizo, aina nne za kasa kuna baadhi ya vyakula wakila wanadamu humsababishia maradhi ama kifo.


Ameeleza kuwa kwa kushirikiana na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bara wamefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini uwepo wa sumu katika nyama hiyo na kusema kuwa sumu hiyo inahimili joto ambapo hata ikipikwa haiwezi kuondoka.


Aidha ameongeza kuwa sumu hiyo kitaalamu inajuulikana kwa jina la telenikostizim ambayo husababisha madhara katika mfumo wa mwanadamu ikiwemo kuhisi kichefuchefu, homa na baadae kufariki.


Kwa upande wake Naibu Mkurugeni Kinga na Elimu ya Afya Fatma Kabole amefahamisha kuwa watoto hao waliofariki wapo chini ya umri wa miaka kumi na wanatoka katika familia tofauti ndani ya Kisiwa panza huku Serikali ikiendelea kufuatilia wengine ili kuwabaini waliotumia nyama hiyo na kuwapatia matibabu.


Amefahamisha kuwa jumla ya watu 160 wanasadikiwa kula nyama hiyo katika kisiwa hicho na kuitaka jamii kuwapeleka katika vituo vya afya kwa uchunguzi na kupatiwa matibabu.


Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 6 Machi kuliripotiwa taarifa za tukio hilo lililotokea katika Kisiwa Panza Mkoa wa kusini Pemba.
Naibu waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akitoa tamko kwa vyombo vya habari kufuatia vifo vya watu 9  vinavyosadikiwa kusababishwa na kula   nyama machi 6 huko kisiwa panza kisiwani Pemba, hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar
 

Mkemia Mkuu wa Serikali  Zanzibar Dkt. Farid Mzee Mpatani akitoa taarifa ya kitaalam kufuatia Vifo vya watu 9  vinavyosadikiwa kusababishwa na kula nyama ya kasa machi 6 huko kisiwa panza kisiwani Pemba, hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar

Naibu Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Fatma Kabole akitoa ufafanuzi wa vifo vya watu 9  vinavyosadikiwa kusababishwa na kula   nyama ya kasa machi 6 huko kisiwa panza kisiwani Pemba, hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja  Zanzibar

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...