Kamishina  wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda, akizungumza   Mafanikio ya TAWA katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri, akizungumza kuhusiana na vikao kazi kati ya Taasisi zilizochini ya Msajili wa Hazina ,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa hilo, Neville Meena, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo


Baadhi ya washiriki katika mkutano wa TAWA na wahariri na waandishi wa habari ,jijini Dar es Salaam.

*Ni mafanikio ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya miaka mitatu

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
MAMLAKA Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan migogoro saba imetatuliwa na kubaki mmoja ambao uko hatua za niwsho.

Migogoro iliyokuwepo ilikuwa ni kikwazo kwa mamlaka kutekeleza majukumu yake huku wananchi wakishindwa kuelewa mipaka ya hifadhi.

Hayo ameyasema Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari juu ya mafanikio ya Miaka Mitatu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika migogoro katika TAWA ilikuwa inanyima usingizi lakini kutokana msukumo wa Rais umewezesha kutatua na kupunguza migogoro ya mipaka ya ardhi kati ya Hifadhi na wananchi.

Amesema TAWA imeendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali yaliyotolewa kupitia Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta waliozunguka katika maeneo yenye migogoro.

Amesema kuwa kwa ushirikiano huo migogoro ya mipaka katika Mapori ya Akiba saba (7) ya Swagaswaga, Mkungunero, Wamimbiki, Igombe, Liparamba, Mpanga Kipengere na Selous kati ya nane (8) yaliyotolewa maelekezo na Kamati ya Mawaziri Nane wa kisekta imemalizika ambapo jumla ya vigingi 1,681 vimesimikwa kuzunguka mipaka ya hifadhi .

Aidha, amesema kuwa katika utatuzi wa migogoro hiyo eneo lenye ekari 103,544.48 limemegwa kutoka kwenye hifadhi na kuwapatia wananchi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, na kwamba Serikali kupitia TAWA inaendelea kukamilisha zoezi la kulipa fidia kaya 145 zilizo katika Pori la Akiba Mkungunero.

Kamishina Nyanda amesema kuwa Mamlaka hiyo imekuwa na mipango ya muda marefu katika ya matumizi ya ardhi katika kutatua migogoro hiyo.

"Tumejipanga na tuna kazi kubwa ya kufanya maeneo hayo ili kuokoa maisha ya watu wasidhurike na wanyama wakali na waharibifu” ameongeza.

Kamishna Nyanda amesema TAWa imejiwekea mipango mikakati imkatika utatuzi wa migogoro hiyo, ambapo eneo la ekari 103,544.48 limetengwa kutoka kwenye hifadhi, na kuwapatia wananchi kwaajili ya shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa hilo, Neville Meena, amesema kutaniko hilo limekuwa na manufaa kwa Wahariri na waandishi kujifunza na kazi mbalimbali za Mamlaka hiyo, huku akiwashauri waandishi kuendelea kujifunza kwa kusoma taarifa mbalimbali za Mamlaka hiyo ili kuwa na wigo mpana wa kuifahamu Taasisi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...