Raisa Said,Tanga

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa 35 ambao wamehukumiwa vifungo mbalimbali kutokana na tuhuma za matukio ya kiuhalifu.

Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika Kipindi cha mwezi mmoja.

Waliofikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo mbalimbali ni pamoja na watuhumiwa wa makosa ya kubaka ,kulawiti, na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ambapo watuhumiwa 20 walipatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo magerezani.

Aidha amesema waliohukumiwa vifungo vya maisha jela ni Deogratius Alex (22),Samweli Ghamuga (25) wote kwa kosa la kubaka huku Athumani Rajab (19) amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti, Anthony Agustino na Twaha Rajabu wamehukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

Watuhumiwa wengine ambao ni Omari- Mganga na Hussein Amiry ( 41) wamehukumiwa kifungo Cha miaka nane jela kwa kosa la wizi pamoja na Salimu Jumbe amehukumiwa miaka 27 jele kwa kosa la kuvunja nyumba na kuiba.

Kuhusu makosa ya usalama barabarani amesema madereva wawili wameondolewa madaraja kwenye leseni zao za dereva na mmoja amefungiwa leseni ya udereva huku wengine wamelipa faini Mahakamani kwa makosa ya ukiukwaji washeria za usalama Barabarani.

Aidha Kamanda wa Polisi Mchunguzi amesema katika Kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Februari 21 Hadi machi 21 ,2024 Jeshi la Polisi Mkoa Wa Tanga limefanikiwa kukamata watuhumiwa 94 wakiwa na makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya uvunjaji ,mauaji,kujeruhi ,kusafirisha wahamiaji haraku ,kujaribu Mali pamoja na kupatikana na silaha sita aina ya Gobole.

Pia alieleza katika kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya wamefanikiwa kukamata wasafirishaji Wa dawa za kulevya aina yabmirungi na wauzaji Wa dawa za kulevya aina ya bhangi ambao ni Godwin Nemes (23) Mkulima Mkazi Wa Rombo Kilimanjaro akiwa na mwezake Christopher John (18) Mkulima Mkazi Wa Rombo ambapo kilo 307.5 za mirungu na kilogramu 73 za bhangi zimekamatwa.

Katika hatua nyingine wamefanikiwa kukamata pikipiki 72 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kutokuwa na namba za usajili ,kutoboa Exos,kutokuwa na leseni nankutovaa kofia ngumu na wengine kujihusisha na vitendo vya kulihaligu.

Amesema kuwa mara baada ya upelelezi kukamilika majalada yatapelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...