Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma
Serikali imesema inaendelea kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya tamaduni kandamizi kwa wanawake pamoja kuendelea kutoa elimu juu ya Mila na Desturi zenye kuleta madhara katika jamii na jitihada mbalimbali zinaendelea ikiwemo mapitio ya Sheria ili kuondokana na sheria kandamizi kwa wanawake na watoto wa kike kwa kuhakikisha wanapata haki na kulindwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia Wanawake na makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima aliyemuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika mkoani humo.
Amesema katika jambo hilo kuna juhudi kubwa na dhamira ya Serikali ambayo imepitisha Muswada wa Sheria ya Uchaguzi ya Vyama vya Siasa ukilenga kutokomeza ukatili mtandaoni dhidi ya wanawake na watoto.
"Serikali ya awamu ya sita imeendelea kufanya jitihada mbalimbali kupitia Wizara yenye dhamana ya masuala ya jinsia kwa Kuendelea kuanzisha na kuimarishwa kwa Madawati ya Jinsia na Watoto katika Vituo vya Polisi ambapo hadi sasa tunayo madawati 420 katika vituo vya polisi" - amesema
Amesema huduma hiyo imewezesha kutolewa taarifa za aina mbalimbali za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watu wazima na watoto, ikiwemo ubakaji, ulawiti, vipigo, ukeketaji, utelekezaji, mimba na ndoa za utotoni;
Kuongeza vituo vya Mkono kwa Mkono (One Stop Centres) vya kutoa huduma kwa Wahanga wa Ukatili wa Kijinsia kutoka 10 mwaka 2017 hadi 21 mwaka 2024 na vituo hivyo vinawezesha utoaji wa huduma rafiki na za haraka kwa waathirika wa vitendo vya ukatili na vinahusisha wataalamu mbalimbali ikiwemo Maafisa wa Jeshi la Polisi, Wataalamu wa Ustawi wa Jamii, Wanasheria na Madaktari kwa ajili ya utoaji wa huduma za matibabu, unasihi, msaada wa kisheria;
Kuanzisha Madawati ya jinsia (295) katika Vyuo vya Elimu ya Juu na Kati katika kuweka namna bora ya kushughulikia changamoto za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye taasisi za elimu na Serikali imeendelea kubuni mbinu za kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa kuanzisha Kampeni ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto iitwayo 'Mimi ni Shujaa, Kataa Ukatili' ambayo inatekelezwa na vijana waitwao SMAUJATA ikiwa na maana ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania.
"Vijana hao ni wazalendo waliojitolea kupinga ukatili huo ambapo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inawalea"
Kuhusu suala la ukatili Waziri Mkuu Majaliwa ametoa rai kwa wananchi wote nchini kupaza sauti na kukemea vitendo vyote vya ukatili kwa wanawake na Watoto na kuendelea kutoa taarifa ya viashiria ya vitendo hivyo kwa mamlaka husika ili kuunga mkono jitihada za Serikali.
Aidha, jamii inapaswa kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika kupiga vita mila na desturi zinazoendelea na kuchochea vitendo vya ubaguzi na udhalilishaji nchini.
Awali kitoa salamu za Mkoa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amesema Dodoma unafanya maadhimisho haya kila mwaka kwani mwaka 2023, yalifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo Wanawake zaidi ya 10,000 waliweza kushiriki.
Aidha, ameongeza kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi kwenye Mkoa wa Dodoma kwani Serikali ya Mkoa Ina viongozi Wanawake kwenye kila nyanja kwa asilimia kubwa. Hii inawapa shime Wanawake kugombea ngazi mbalimbali za uongozi Serikalini.
Sanjari na hayo, uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Jinsia na maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2023 umefanyika.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani (SWD) yalianza mwaka 1911 kufuatia maandamano ya Wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kupinga mazingira duni ya kazi kama vile ukosefu wa huduma za kijamii na uwepo wa vitendo vya unyanyasaji katika ajira.
Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine ilianza kuadhimisha siku hii mwaka 1997. Mwaka 2005, maadhimisho yameendelea kufanyika kila mwaka kwa ngazi ya Mkoa na yale Kitaifa hufanyika kila baada ya miaka mitano (5). Maadhimisho ya mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu inayosema "Wekeza kwa wanawake: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii".

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...