WANUFAIKA 08 Wa Ruzuku ya Mradi wa "Fee Free" uliopewa ufadhili na Balozi wa Norway na Ubalozi wa Uswisi wafanya Maonesho ya kazi zao za Sanaa huku wamewasihi vijana kutuma maombi ya kupata Ruzuku ili kufanya kazi zao za kisanaa kwa weledi.

Akizungumza wakati wa Kutambulisha kazi hizo Mkurugenzi wa Nafasi arts space Lilian amesema amefarijika sana Kuona Wanawake wengi wamefanya miradi ya kiujasiriamali ili kuwapa motisha Wanawake waliokosa ajira kuona ipo fursa ya kuchangamkia fursa mbalimbali kupitia vipawa vyao.

"Sisi kama Nafasi arts space tunapenda zaidi kufanya kazi watu wenye bunifu zaidi za kazi za kisanaa na tunawapa kipaumbele zaidi hasa Vijana wadogo ,Walemavu na kundi maalum kwani tuna amini katika bunifu zao ."

Aidha amesema Mradi huo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway pamoja na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania umehaidi kuendelea kushika mkono vijana wenye wazo la kibunifu kupitia Sanaa.


Aidha ameongeza kuwa Nafasi itatumia fursa hiyo kutoa msaada kwa wachache watakaochaguliwa ili kuendelea kutoa miradi ya ubunifu za kisanaa itakayowanufaisha wasanii wa Kitanzania sambamba na hadhira yake.

Pia ametoa wito kwa vijana kukimbilia fursa ya kutuma maombi ya ruzuku hiyo kwa msimu mwingine kwa Nafasi art space ina amini katika kuendeleza na kurutubisha uwezo wa watu kupitia njia ya Sanaa za kisasa.


Kwa upande wake Mnufaika wa Ruzuku hiyo Scholastica Sultan amesema wazo lake yeye la kisanaa "Ndoto ya Kalista" lililenga wasichana wadogo na Wanawake ambao wametelekezwa na Wanaume wao(single mother) ambao wamekata tamaa ya kimaisha kutokana na kukosa msaada upande wa mzazi mwenzie nakuona ndoto za kujikwamua kiuchumi zimeishia hapo.

"Tulikuwa na mradi kazi ambao ulilenga pishi la Keki ambapo ndani yake kulikua na masimulizi y namna changamoto wanazopitia Wanawake hao ambapo tulifanya simulizi kutoka Jijini Dar es Salaam pamoja na Mkoa wa Tanga ."

Pia ameeleza kuwa katika mradi kazi huo Umeweza kutoa taswira mpya kwa Wasicha hao na kuona fursa ya upishi wa keki utaweza kuwapatia kipato kupikwa kiuchumi na kulea watoto wao .





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...