CHUO Kikuu Mzumbe kimeendelea kuwanoa watumishi wake kuhusu matumizi ya Mfumo Mpya wa manunuzi kwa umma kwa njia ya mtandao (National e-Procurement System of Tanzania-NeST) ili waweze kutimiza majukumu yao kwa wakati kwani mfumo huo ni wa wazi na manunuzi yote hufanyika ndani ya mfumo.

Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Jones Mapande ambaye ni Afisa Manunuzi Mwandamizi amesema , mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kuwa na utaratibu mzuri wa ununuzi wa huduma na bidhaa na kazi kwa njia inayostahili kwa kutumia mfumo huo mpya wa manunuzi.

“Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watumishi wote wanahusika na ununuzi ambao hapo awali hawakupata mafunzo hayo au wamekutana na changamoto mbalimbali waweze kupata uelewa wa matumizi ya mfumo huo” Alisisitiza Bw. Mapande.

Aidha Bw. Mapande aliongeza kuwa ni wajibu wa kila Mtumishi anaye husika na ununuzi kuujua mfumo wa NeST ipasavyo kwani mfumo huo una faida mbalimbali kama vile kuharakisha mchakato wa ununuzi, kuondoa manung'uniko kwani ni mfumo wa wazi na pia unasaidia kupata thamani ya fedha kwa manunuzi yanayofanyika.

Mafunzo hayo ya siku nne yaliyoanza leo Machi 25 hadi 28, 2024, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam yanashirikisha watumishi kutoka idara na vitengo mbalimbali.

Chuo Kikuu Mzumbe kimeanza kutumia mfumo Mpya wa manunuzi kwa njia ya Mtandao tangu Oktoba Mwaka jana.
Washiriki wa Mafunzo ya Matumizi ya mfumo  mpya wa manunuzi ya Umma (NeST) wakifuatilia mafunzo hayo.

Mkufunzi wa Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo mpya wa Manunuzi ya Umma(Afisa Manunuzi Mwandamizi) Janes Mpande akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Tehama Chu Kikuu Mzumbe, Joseph Kiphizi akieleza namna ya Kutumia mfumo  mpya wa manunuzi ya Umma (NeST).
Watyumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiendele kunolewa juu ya mfumo  mpya wa manunuzi ya Umma (NeST) 
Mkufunzi wa Mafunzo ya mfumo  mpya wa manunuzi ya Umma (NeST),Hussein Kiboko akifafanua jambo.
Wakufunzi wa Mafunzo ya mfumo  mpya wa manunuzi ya Umma (NeST) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...