Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kutowapatia kazi za usimamizi wa miradi Wahandisi Washauri wanaoshindwa kuwasimamia Wakandarasi kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kwa viwango na mujibu wa mikataba na kupelekea Mkandarasi kurudishwa eneo la mradi kurudia kazi.

Bashungwa ameagiza hayo Machi 22, 2024 Wilayani Mafia wakati akikagua barabara ya Kilindoni - Utende (km 14.6) kwa kiwango cha lami, iliyojengwa na Mkandarasi CHICO na chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri Kampuni ya UWP Tanzania ambapo barabara hiyo haikutekelezwa kwa viwango na kusababisha Mkandarasi kurudia sehemu ya kazi.

“Kama mlivyofanya katika mradi huu kwa kumrudisha Mkandarasi Site, Wahandisi Washauri kama hawa wanaoshindwa kumsisimamia Mkandarasi wanapaswa wawe ‘blacklisted’ kwa sababu tunawalipa pesa ya kumsimamia Mkandarasi kwaniaba ya Serikali”, amesema Bashungwa.

Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kutompatia kazi yoyote ya kusimamia miradi Mhandisi Mshauri wa kampuni ya UWP Tanzania na wahandisi washauri wengine wa aina hiyo ambao wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa kuwasimamia Makandarasi kutekeleza miradi kikamilifu na kuisababishia hasara Serikali.

“Mhandisi Mshauri UWP hafai na nikiona mmempa kazi sehemu yotote mimi na nyinyi na hii iwe funzo kwa Wahandisi Washauri wengine tunaowapa kazi ya kuwasimamia Makandarasi”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema kuwa Wizara ya Ujenzi itaendelea kuwasimamia Wakandarasi na Wahandisi Washauri walipatiwa kazi za kutekeleza miradi ili fedha zinazotolewa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ziweze kutekeleza na kukamilisha miradi kikamilifu kama ilivyokusudiwa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS Eng. Malima Kusesa ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Kilindoni - Utende (km 14.6) kwa kiwango cha lami ulikamilika mwaka 2015 na baada ya muda wa matazamio 2016 yalibainika mapungufu katika kipande cha kilometa nne.

Eng. Kusesa ameeleza kuwa baada ya kubainika mapungufu hayo,TANROADS walimtaka Mkandarasi CHICO na Mhandisi Mshauri UWP Tanzania kurudia kazi sehemu hiyo kwa gharama zao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...