Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) leo tarehe 15 Machi, 2024 amefanya ziara ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika Mkoa wa Mara.

Mhe. Nape ameongozana timu ya wataalam wa wizara pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ambazo ni Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Kupitia ziara hiyo, Wizara inaendelea kuhamasisha juhudi za kuboresha mawasiliano nchini kote, kuzingatia malengo ya kuwa na mawasiliano nchi nzima na kufanikisha lengo la Tanzania kuwa nchi ya kidijitali. Hii ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano na kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano zinapatikana kwa wananchi wote.

#MawasilianoNchiNzima #TzyaKidijitali #KaziIendelee
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...