NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imefanikiwa kukamata Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya aina ya methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu.

"Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, heroin na methamphetamine". Amesema

Amesema, dawa hiyo ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majina bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy.

Aidha amesema wamefanikiwa kukamata jumla ya Kilogramu 54,506.553 za dawa za kulevya za mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi.

Amesema watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

"DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wakala wa misitu (TFS) tulifanya operesheni katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata dawa hizi". Amesema.

Amesema dawa zilizokamatwa ni bangi kilo 54,489.65, mirungi Kilogramu 10.3, heroin gramu 90.93, cocaine gramu 1.98 na Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za DCEA leo  Aprili 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...