Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na nderemo na wananchi wa Mbarali, wakiongozwa na vijana waendesha bodaboda, baada ya kuwasili na msafara wake katika Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, leo Aprili 18, 2024, akitokea Mbeya Mjini.

Dk Nchimbi alisimama kuwasalimia wananchi hao wa Ubaruku, akiwa njiani kuelekea Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndg. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...