Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma
Hospitali ya Benjamin mkapa jijini Dodoma imewakumbuka watoto yatima wanaoishi Katika kituo cha kulelea watoto Yatima cha Rahman kilichpo kata ya cha Chang'ombe jijini Dodoma.
Kituo hicho kimepaitwa msaada kutoka hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha tabasamu na kuwafafiji watoto hao katika sikukuu ya Eid.
Msaada huo umekabidhiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) Dkt Alphonce Chandika ni pamoja na mbuzi wawili, kilo 50 za mchele, kilo 50 za unga wa ngano, juisi katoni 10 na maji katoni 20 ya kunywa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo, Dkt Chandika, amesema pamoja na kutoa huduma za afya, lakini wana wajibu wa kurudisha kwa jamii na kulea jamii inayowazunguka.
"Leo tumeona tuwakabidhi watoto yatima vyakula kama mkono wa Eid-el-Fitr ili nao waweze kusherehekea sikukuu kama watoto wengine," amesema Mkurugenzi Mtendaji, wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vyakula hivyo.
Katika makabidhiano hayo Dkt.Chandika aliambatana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Hospitali, Prisca Lwangili, na Mwanasheria wa Hospitali, Advocate Alfred Kanan.
Awali akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaada huo Mkurugenzi wa Kituo Rukia Hamis, anasema Kituo kilianza mwaka 1998 kwa ajili ya kutatua changamoto za kinamama.
"Mwaka 2006, tukaona pia tutoe malezi kwa watoto wanaopitia changamoto hivyo tukaanza na watoto 15, Sasa hivi tuna watoto 150," anasema.
Rukia ameishukuru BMH kwa msaada huo na kuziomba taasisi nyingine ziige mfano wa BMH kwa kuwakumbuka watoto yatima nyakati za sikukuu ili watoto hao nao waweze kufurahi kama wengine.
Home
JAMII
HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE MAHITAJI KITUO CHA RAHMAN CHANG'OMBE - DODOMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...