Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu  kuendelea  kutenda mema , kuombeana baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na  kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu.

Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipotoa zawadi za mkono wa Eid alipotembelea vituo mbalimbali vya kuwalea Wazee na Watoto ikiwemo kituo cha kulea Watoto  ZASO Fuoni Mambosasa,  kituo cha Wazee Welezo , kituo cha Wazee Sebleni , kituo cha  Watoto SOS na kituo cha  Watoto Mazizini , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 10 Aprili 2024.

Aidha Mama Mariam Mwinyi amesema ni wajibu kuwalea, kuwatembelea na kuwaenzi Wazee kufanya hivyo ni baraka kubwa sana.

Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwasaidia Wazee na kuwajali.








 

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...