Wakiwa kwenye picha ya pamoja ni ujumbe kutoka Uganda, wakiwemo wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda. Katikati ni Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Mwenyekiti wa Kamati; na kushoto kwakwe ni Prof. Lughano Kusiluka, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (aliyevaa Kaunda).

.......

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, ya Bunge la Uganda imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, pamoja na kusifu Amani na Utulivu mkubwa uliopo, kwa kuzingatia idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Alhamisi tarehe 18 Aprili 2024, walipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho pamoja na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, kwenye ofisi yake iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dodoma.

Aidha, wamevutiwa na aina ya masomo yanayofundishwa katika Ndaki, Shule Kuu na Taasisi za Chuo, pamoja na namna chuo kinavyoendelea kuwekeza katika kuanzisha programu mpya za masomo zinazoakisi mabadiliko makubwa ya kisekta yanayozingatia utoaji mafunzo wenye kutatua changamoto kubwa za ajira, na matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.

Akiukaribisha ujumbe huo, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Kusiluka amelishukuru Bunge la Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwaleta wabunge hao kuja kujifunza UDOM, na kueleza ni kwa namna gani wabunge hao wana mchango mkubwa katika kuongeza hamasa ya ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kutunga Sera zenye kusaidia nchi hizo kuendana na mabadiliko makubwa ya kisanyansi na teknolojia katika Sekta ya Elimu.

Aidha, amewahamasisha waganda kuja kusoma Tanzania kutokana na uwepo wa mitaala mizuri na masomo yenye kukidhi mahitaji katika soko la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Tunayo fursa ya wananchi wa Uganda na nchi nyinginezo za Afrika Mashariki kuja kusoma UDOM. Niwahakikishie tunayo mazingira mazuri na thabiti ya kujifunzia kwa wana Afrika Mashariki kuja kusoma Tanzania. Mazingira yetu, tamaduni na mahitaji yetu yanafanana, kwangu mimi hii ni fursa kwetu sote” alisisitiza

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo waliofika kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma ni pamoja na Mhe. Betty Ethel Naluyima, Mhe. Dkt. Isingoma Patrick Mwesigwa, Mhe. Rwemulikya Ibanda Gerald, Mhe. Patrick Ocan na Mhe. Lillian Obiale Paparu.Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda, wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, ofisini kwake Dodoma.Wakiwa kwenye picha ya pamoja ni ujumbe kutoka Uganda, wakiwemo wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, wa Bunge la Uganda. Katikati ni Mhe. Gilbert Olanya, wa Jimbo la Kilak Kusini, Mwenyekiti wa Kamati; na kushoto kwakwe ni Prof. Lughano Kusiluka, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (aliyevaa Kaunda).Prof. Lughano Kusiluka akikamkabidhi zawadi ya ukumbusho Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Uganda, Mhe. Gilbert Olanya. Wabunge hao walifika kutembelea chuo na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu utoaji wa Elimu ya Juu nchiniTanzania.Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiagana na waheshimiwa wabunge wa Uganda, baada ya kuhitimisha ziara yao chuoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...