

Akizungumza leo Aprili 18, 2024 na Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dkt. Jackson Chiwaligo amesema hiyo ni mara ya kwanza kufanya upasuaji kama huo.
Dkt. Chiwaligo ameeleza kuwa mgonjwa huyo alifika Hospitali ya Sekoutoure akiwa na changamoto ya kupata maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo kwa zaidi ya miaka mitatu.
“Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya kibofu cha mkojo ulisababisha kufanyiwa upasuaji na kuondoa lenye uzito wa Gramu 800”, amebainisha Dkt. Chiwaligo
Dkt. Chiwaligo ambaye aliwaongza madakatafi wenzake amesema uwepo wa jiwe kwenye kibofu ni mkusanyiko wa madini ya chumvi ambayo hukauka na kusababisha uvimbe kutokea katika kibofu cha mkojo.

“Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni kwenda haja ndogo kwa wakati pale unapoipata na kunywa maji ya kutosha kwa wakati ” , ameeleza Dkt. Chiwaligo
Dkt. Chiwaligo ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu wa kufika hospitalini kupata huduma za vipimo na kuwa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka changamoto ya magonjwa kama hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...