Na Nasra Ismail, Geita

MBUNGE  wa Jimbo la Busanda Tumaini Magesa ameahidi ndani ya mwezi mmoja na nusu anatarajia kukamilisha ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Lutozo iliyopo katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro mkoani Geita.

Ametoa ahadi hiyo leo aliposhiriki kuchimba msingi wa bweni hilo ambalo linatakiwa kutumika katika msimu mpya wa masoma ya kidato cha tano mwaka huu.

Shule ya Sekondari Lutozo imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa takribani miaka 5, hivyo kufanya shule hiyo kupata hadhi ya kuwa na masomo ya kidato cha tano na cha sita.

Magesa pia alipata wasaa wa kusikiliza kero za wananchi ambapo kero kubwa ni utiririshwaji wa maji yenye kemikali kutoka kwenye maplanti kwenda kwenye mito ya maji ya matumizi ya binadamu.

Ambapo Mbunge Magesa ameahidi kuita wataalam kupata majibu kuhusu  usalama wa maji na pia kuongea na wamiliki ili waweze kuzuia utiririshwaji huo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Katoro Kigongo Benedict Sweya amemshukuru na  kumpongeza mbunge huyo kwa kutoa Sh.5 kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni hilo.

"Matarajio ni kwamba mwaka huu tunaenda kupokea watoto wa kidato cha tano nina imani  umewapigia wadau na wamekubali kushiriki  kwani wana imani kubwa na wewe Mbunge wetu na  ndani ya mienzi hiyo ujenzi utakuwa umekamilika,"Kigongo.

Aidha amemuomba mbunge kuwasaidia kupata kisima cha maji katika shule hiyo kwani imekuwa changamoto kubwa.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...