Zaidi ya shilingi Bilioni 15 zimetolewa na Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kuchangia ukuaji wa sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato wakati akiwautubia wananchi wa manispaa ya Bukoba kwenye Mkutano wa hadhara umefanyika katika viwanja vya Soko kuu la Manispaa hiyo tarehe 14 April, 2024.

Wakili Byabato amesema kuwa katika miaka 3 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo inahitimishwa mwezi huu serikali ya awamu ya 6 imetoa fedha nyingi ambazo zilisaidia kuboresha mindomibinu ya elimu, Barabara, huduma za afya na Uchumi kwa wakazi wa Jimbo la Bukoba mjini, Amesema kuwa kupitia fedha hizo baadhi ya maeneo ambayo hayakuwa na shule yamepata huduma hiyo kwa kujengewa shule mpya za msingi na sekondari sambamba na kuanzisha huduma za Viwanda, Biashara na uwekezaji.

Miradi mingine ya mafanikio ni pamoja na uwekaji wa Taa za Barabarani, Marekebisho katika Soko kuu, Usafishaji wa mto Kanoni, Ujenzi wa Hospitali ya wilaya iliyopo Nshambya pamoja na uunganishaji umeme kwa wananchi kupitia miradi inayotekelezwa na wakala wa umeme vijijini - REA.

Kufuatia kuwepo kwa mafanikio hayo sambamba na uwepo wa mahitaji mengine ya maendeleo, Wakili Byabato ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa .

Wakati huo huo Wakili Byabato amezindua ligi ya Mpira ambapo ametoa mipira minne kwa kila kata pamoja na kiasi cha shilingi laki mbili ambazo zimekabidhiwa kwa Madiwani wa kata zote 14 za Jimbo hilo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ligi hiyo Pia amekabidhi rasmi kwa wananchi gari la wagonjwa ambalo lilitolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba wamemshukuru Mheshimiwa Rais pamoja na Mbunge kwa jinsi wanavyopambana kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa kiuchumi kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...