LIGI ya mabingwa ulaya hatua ya nusu fainali kurindima wiki hii ambapo miamba minne ya soka itacheza michezo yao ili kujikatia tiketi ya kufuzu fainali ya michuano hiyo itakayopigwa katika dimba la Wembley nchini Uingereza.

Vilabu hivo vinne vitakavyokua vinawania tiketi ya kwenda Wembley ni Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani ambao wao leo watakipiga na Real Madrid katika nusu fainali ya kwanza, Huku ndugu zao kutoka Ujerumani klabu ya Borussia Dortmund wao watakipiga dhidi ya mabingwa wa Ufaransa klabu ya PSG katika nusu fainali ya pili kesho Jumatano.

Nusu fainali ya kwanza leo ambayo itawakutanisha miamba ya soka barani humo klabu ya Bayern Munich bingwa mara sita wa michuano hiyo akicheza na Real Madrid bingwa mara kumi na nne wa michuano hiyo, Unatarajiwa kua mchezo mkali kutokana na ubora wa vilabu hivo.

Mchezo kati ya Bayern Munich na Real Madrid ni mchezo wenye hadi kubwa sana barani ulaya mara nyingi wanapenda kuuita European Clasico kwa maana vinakutana vilabu ambavyo vina historia kubwa kwenye michuano hiyo mikubwa kabisa barani humo.

Vilabu hivo vimekutana mara 26 kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kushinda mara 12, Huku Real Madrid wakishinda mara 11 na mchezo huo ukimalizika kwa sare mara 3, Bayern Munich wakifunga mabao 41 Real Madrid wao wakifunga mabao 39.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya nusu fainali itakayopigwa leo Jumanne na kesho Jumatano. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Mchezo mwingine wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya  ambao utarindima ni kati ya klabu ya Borussia Dortmund dhidi ya klabu ya PSG kutoka kule nchini Ufaransa ni mchezo ambao pia unatazamiwa kua na uhsindani mkubwa, Kwani vilabu hivyo vyote vimeonesha ubora mkubwa mpaka kufikia hatua hii.

Borussia Dortmund wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuwapa kipigo cha kushangaza klabu ya Atletico Madrid, Kwani mchezo wa kwanza Atletico walipata matokeo ya ushindi wakiwa nyumbani mabao mawili kwa moja lakini Dortmund walipindua meza wakiwa katika dimba la nyumbani na kushinda kwa mabao manne kwa mawili.

PSG wao stori yao inafanana na ya wapinzani wao Dortmund kwani mchezo wa kwanza walipoteza nyumbani kwa mabao mawili kwa moja mbele ya Barca, Lakini walienda ugenini na kufanikiwa kupindua meza na kupata ushindi wa mabao manne kwa moja na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali.

Vilabu hivi vimefanikiwa kukutana mara nne tu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya ambapo klabu ya Borussia Dortmund wakipata ushindi mara moja, Huku klabu ya PSG wao wakipata ushindi mara mbili na mchezo huo ukimalizika kwa sare mara moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...