Na Mwandishi Wetu,Michuzi Tv

Rais Samia hahusiki na sadaka ya Sh 5,000 Pemba, ni upotoshaji
MKUU wa Mkoa Kusini Pemba, Amour Hamad Salehe, amekanusha taarifa za uzushi zilizosabazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa sadaka ya Sh 5,000.

Amesema taarifa hizo ni uzushi na upotoshaji kwa sababu zoezi hilo halihusiani kabisa na Rais Samia kama inavyopotoshwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna mfanyabiashara mmoja amekuwa na utamaduni zaidi ya miaka sita wa kutoa sadaka kwa watoto mayatima kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kwa awamu ya kwanza zoezi la utoaji sadaka lilifanyika kwa ufanisi mkubwa. Awamu ya pili wananchi walipeana taarifa iliyohamasisha wananchi kufika kwa wingi. Waliokuwapo kwenye mpango walipata sadaka kama ilivyopangwa.

Kwa ubinadamu wake wote waliokuwa nje ya mpango walipewa kila mmoja Sh 5,000 kama nauli ya kurejea nyumbani na sio sadaka,” Alisema RC Amour.

Aidha katika hatua nyingine, mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa jina la Abas Haji anayemiliki hoteli kwenye eneo la Mgogoni Pemba, alisema “msaada huu sio kutoka kwa Mama Samia wala Ikulu au watu wengine. Msaada huu ni mimi kama mimi na familia yangu,”




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...