Rukwa

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara, vivuko na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani Rukwa ili kuinua shughuli za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa TARURA Mkoa wa Rukwa, Mhandisi William Lameck alisema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara za wilaya nchini.

Mhandisi Lameck amemshukuru Rais Samia kwa kuongeza bajeti ya TARURA Mkoa wa Rukwa kutoka Shilingi Bilioni 5.63 hadi kufikia Shilingi Bilioni 12.3 ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuimarisha mtandao wa barabara mkoani humo.

"Barabara kwa kiwango cha changarawe zimeongezeka kutoka Km 867.25 hadi Km 1,143.05," alibainisha.

“Tumeongeza mtandao wa barabara za lami na kufanyia matengenezo ya kawaida maeneo korofi jumla ya Km 196.66, ujenzi wa lami Km 0.8 na zege Km 1.55 zitatengenezwa katika Manispaa ya Sumbawanga na Wilaya ya Kalambo na Nkasi", alisema.

"Pia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe Km 179.5 na ujenzi wa daraja la Kavunja lenye urefu wa mita 39 linalounganisha vijiji vya Kirando, Kazovu na Korongwe wilayani Nkasi lenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.76 ambapo ujenzi wake umekamilika na daraja linatumika.

Amesisitiza daraja hilo limepunguza gharama za usafiri na usafirishaji ambapo hapo awali wananchi walikuwa wanazunguka katika vijiji vya Wilaya ya Kalambo lakini sasa wanatumia daraja hilo bila kuwa na wasiwasi juu ya mali zao na usalama wao.

Mkazi wa Nkasi Bi. Sarafina Mbalamwezi ameipongeza kwa kile inachokifanya kuhakikisha miradi ya barabara inatekelezwa na kukamilika kwa wakati na wananchi kuondokana na changamoto ya barabara.

Alisema uboreshaji wa miundombinu ya barabara umeweza kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma mbalimbali ikiwemo ya matibabu.

Mkazi wa Sopa wilayani Kalambo, Bw. Amon Kabwe amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuboresha miundombinu vijijini ili kuhakikisha wananchi wanasafiri na kusafirisha mazao yao sokoni kwa urahisi," alisema.

Alisema hapo awali kulikuwa na changamoto ya barabara kutopitika hasa kipindi cha masika lakini kwa sasa barabara hizo zinapitika muda wote na madaraja korofi yametengenezwa na yote yanatumika.

Muonekano wa barabara ya Malichewe yenye urefu wa Km. 1.2 katika wilaya ya Sumbawanga ambapo ujenzi wake umekamilika.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...