
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Tree Oceans Ltd . Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE Naseem Allan (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi waliojishindia kwenye mchezo wa VUNADEILE kulia ni Mratibu kutoka BBT Vumilia Zikankura hafla yakukabidhi zawadi hizo umefanyika jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Three Oceans Ltd. Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashili wa VUNADEILE imesema itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha Vijana kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri.
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar Salama es Salaam na Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Mawasiliano kutoka kwenye kampuni hiyo Naseem Allan wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wanaopatikana kila siku kwenye droo ikiwemo gari mpya kabisa aina ya Toyota Ist, pikipiki, tv na simu janja aina ya Samsung na iphone 15.

Ameeleza kuwa katika kuendesha bahati nasibu hiyo kampuni inashirikiana na Mradi wa kilimo ili kuhakikisha tunawawezusha vijana-BBT ni Taasisi iliyopo chini ya wizara ya kilimo yenye lengo kuu la kutoa hamasa kwa Vijana kujikita kwenye shughuli za kilimo biashara Ili waweze kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu kutoka BBT Vumilia Zikankura amebainisha kuwa BBT imekuwa ikiwawezesha Vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo biashara kwa kuwawezesha mitaji na Masoko huku akiwataka Vijana kujitokeza kwenye program ya BBT na VUNA DEILE Ili waweze kujishindia Zawadi mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...