Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika mapokezi ya viongozi wa dini waliosafiri kwa treni ya mwendokasi wakitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024.

Viongozi hao wanatarajia kushiriki ibada maalumu ya kuliombea Taifa itakayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Aprili 22, 2024 na kuongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Akizungumza mara baada ya treni hiyo kuwasili, Dkt. Jafo amesema hiyo ni fahari kubwa kwa nchi yetu kupata usafiri huo ambao pamoja ya kwamba unatumia muda mfupi kusafiri lakini pia umewaunganisha Watanzania wote kwani kuna wengine wametoka Pemba na Unguja.

Amesema wakati Taifa linaelekea kuadhimisha miaka 60 ya Muungano hayo ni mafanikio makubwa katika sekta ya usafiri kwani kupitia Muungano wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar wanajenga uchumi kwa mafanikio makubwa ya nchi.

Dkt. Jafo ameongeza kuwa kwa vile Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa reli ya kisasa imeona ni jambo la heri viongozi wa dini wawe wa kwanza kupanda chombo hicho wakati wanakwenda kuliombea Taifa.

Amesema Tanzania ni Taifa la mfano duniani ambalo wananchi wake kutoka Bara na Zanzibar wameungana na kujenga uhusiano wa damu ambao umedumu kwa kipindi kirefu.

“Ndugu zangu najua mmetoka mbali tunawakaribisha sana Dodoma, lakini naomba niwaambie viongozi wa dini Serikali inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inawapenda sana na kesho tutakuwa na maombi ya kuliombea Taifa letu kwa tunu ya Muungano tuliyonayo,” amesema.

Akielezea namna maadhimisho hayo yatakavyoadhimishwa, Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali imeamua kufanya maombi maalumu tarehe 22 na tarehe 24 kutakuwa na tuzo maalumu kwa waasisi wa Muungano, tarehe 25 kutakuwa shamrashamra za Muungano jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na kielele cha maadhimisho hayo Aprili 26, 2024.

Miongoni mwa waliosafiri na treni hiyo kutoka jijini Dar es Salaam ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Viongozi walioshiriki katika mapokezi hayo ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati wakisubiri treni ya majaribio iliyobeba viongozi wa dini waliosafiri kwa treni ya mwendokasi wakitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiongoza viongozi na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika mapokezi ya treni ya mwendokasi ya majaribio iliyobeba viongozi wa dini waliosafiri kwa treni ya mwendokasi wakitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisalimiana na viongozi wa dini wakati wakiwasili mkoani wakitokea Dar es Salaam kwa treni ya kisasa ya mwendokasi ikitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wakati wa mapokezi ya treni ya mwendokasi iliyobeba viongoza wa dini waliowasili mkoani Dodoma wakitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma SACP Theopista Mallya mara baada ya mapokezi ya treni ya mwendokasi iliyobeba viongoza wa dini waliowasili mkoani Dodoma wakitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule mara baada ya mapokezi ya treni ya mwendokasi iliyobeba viongozi wa dini waliosafiri wakitokea Dar es Salaam leo Aprili 21, 2024 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa maelezo kuhusu kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais kabla ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Aprili 24, 2024.
 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa utambulisho mfupi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Aprili 24, 2024.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na mawaziri mbalimbali hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Aprili 24, 2024.
 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Aprili 24, 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...