Kwa kujibu maoni ya wateja, Kampuni inayoongoza kwa mahitaji ya usafiri kwa njia ya mtandao Bolt, itapanua huduma zake za kupangilia safari (pre booking) kwa wateja. 

Sasa wateja wote wa makampuni wanaweza kupangilia (kufanya booking kabla) safari zao hadi siku 90, ikilinganishwa na utaratibu wa awali wa masaa 72.

Uamuzi huu unakuja huku Bolt ikipata ongezeko kubwa la mahitaji ya safari zilizoratibiwa na kiwango cha ukuaji cha mwezi baada ya mwezi kwa asilimia 30%.

Upanuaji kwa kiwango cha juu kuhusu upangliaji wa safari zilizoratibiwa kunalenga kuboresha hali ya utumiaji kwa wateja, hasa kwa wateja wa makampuni na biashara za kati, kwa kuwawezesha kupanga safari zao mapema.

Zaidi ya hayo, wateja sasa wana chaguo la kuchagua aina wanayopendelea ya usafiri na kutoa maagizo mahususi kwa madereva, hivyo kuruhusu hali ya utumiaji liyobinafsishwa zaidi kulingana na mahitaji ya mtu binafsi.

Uboreshaji huu unasaidia malengo ya kuokoa muda kwa makampuni na SMEs.Milu Kipimo, Country Manager wa Bolt Business nchini Tanzania & Tunisia alisema: "Tumeona mahitaji makubwa ya safari zilizoratibiwa tangu tulipoanzisha huduma hii mwaka wa 2022 ili kujibu maoni ya wateja.

Kwa kuongeza muda wa kupangilia na kuratibu mapema kutoka saa 72 hadi siku 90, tunatumai kuona mafanikio zaidi na chanya kwa makampuni.

Ni hatua nyingine kuelekea dhamira yetu ya kuwezesha wateja wetu wa biashara/makampuni kupanga na kujua safari zao kwa ufanisi.

Bolt inasalia na nia ya kuendelea kutafuta njia za kuinua hali ya matumizi ya jumla ya mtumiaji kwenye app yake, kwa kuvumbua na kutumia uwekezaji wa kimkakati ili kutoa matumizi ya bei nafuu, rahisi na ya kufurahisha kwa watumiaji wote.

Mapema mwezi huu Bolt ilitangaza Kuponi za Bolt Business ili kuwezesha makampuni kushiriki au kulipia kikamilifu gharama ya safari moja kwa wafanyakazi na wateja wao, kuimarisha urahisi na ufanisi katika safari za kikazi.

Sehemu ya jukwaa la Bolt Business, kuponi hukidhi mahitaji mbalimbali ya usafiri wa kikazi, ikiwa ni pamoja na safari hadi matukio ya kikazi ya kampuni, vifurushi vya manufaa ya mfanyakazi, na kuimarisha kuridhika kwa mteja.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...