NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

 

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amewasihi Wananchi wa Jimbo la Kwahani kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM kwani ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa vitendo.

 

Nasaha hizo amezitoa wakati akizindua kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo katika Uwanja wa Tawi la CCM Sebleni Zanzibar.

 

Alisema CCM imejipanga kuhakikisha mgombea wake anashinda katika Uchaguzi huo ili kuendeleza maendeleo na ustawi wa jamii katika Jimbo hilo ambalo ni ngome ya CCM toka kuanzishwa kwa mfumo wa Vyama vingi vya  siasa nchini.

 

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa,amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi amefanya kazi kubwa na nzuri,hivyo anastahili kupewa Viongozi imara na makini wanaotokana na CCM ili wamsaidie kazi.

 

" Maendeleo ya Jimbo hili yatazidi kuimarika zaidi chini ya Viongozi wachapakazi,waadilifu na wachapakazi wanaojali utu na maisha ya Wananchi wote bila ubaguzi wa kisiasa,kikabila na kidini na kazi hiyo ataifanya kwa ufanisi mkubwa ndugu yetu Khamis Pele." alisisitiza Dkt.Dimwa.

 

Akizungumzia mafanikio ya CCM katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 uliofanyika katika Jimbo la Kwahani ikiwemo ujenzi wa Skuli ya kisasa ya ghorofa Shehia ya  Muungano iliyogharimu zaidi ya Bilioni 6.1,ujenzi wa Soko la Kwahani uliogharimu kiasi cha zaidi ya milioni 500, wanufaika wa miradi wa TASAF ni 242 unaogharimu zaidi ya milioni 577.4 pamoja na utoaji wa Pencheni Jamii kwa Wazee 582.

 

Pia utekeleza wa Ilani ya CCM kwa upande wa Mbunge na Mwakilishi wameimarisha sekta za Elimu,afya,maji safi na Salama, ujenzi wa Ofisi za CCM ngazi zote,vikundi vya ujasirimali, ununuzi wa vifaa vya michezo na misaada ya Kijamii kwa Wananchi vilivyogharimu shilingi 467.8.

 

Kupitia Mkutano huo Dkt.Dimwa, alimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea huyo Khamis Yussuf Mussa (Pele), na kumsisitiza kuwa ilani hiyo ndio mkataba kati ya wananchi na CCM hivyo akishinda kazi kubwa ya kuendeleza maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

 

Kampeni hizo za Uchaguzi huo zinafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ahmada Yahya Abdul Wakil (Shaa) tarehe 8,April 2024 kwa maradhi ya shinikizo la damu, na Uchaguzi huo umepangwa kufanyika June 8, mwaka 2024.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa (kulia), akimkabidhi Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 Mgombea nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani (kushoto) Khamis Yussuf Mussa(Pele) katika uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika Uwanja wa Ofisi ya Tawi la CCM Sebleni Zanzibar leo Mei 26, 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...