Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Kapteni Mstaafu George Mkuchika (Kushoto) sambamba na  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NBC, Dk. Elirehema Doriye (wa pili kushoto) wakikabidhi kombe la Ligi Kuu ya NBC kwa nahodha wa timu ya Yanga SC Bakari Mwamnyeto (Kulia) baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2023/2024. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wakati wa mechi ya ligi hiyo baina ya mabingwa hao dhidi ya Tabora United iliyoisha kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3 -0.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Waziri Barnabas (kushoto) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa Yanga Aziz Ki aliyetangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa mwezi wa April. Makabidhiano hayo yalifanyika mapema kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga SC dhidi ya Tabora United uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ukienda sambamba na hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Yanga. Mechi hiyo iliiisha kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3 -0.

Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa Yanga Aziz Ki aliyetangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa mwezi wa April. Makabidhiano hayo yalifanyika mapema kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga SC dhidi ya Tabora United uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ukienda sambamba na hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Yanga. Mechi hiyo iliiisha kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3 -0.Katika kufanikisha hafla hiyo mwishoni mwa wiki benki ya NBC mbali na kushirikiana na timu ya Yanga SC kufanikisha baadhi ya matukio ikiwemo burudani kwenye mkesha maalum wa ubingwa, kuandaa helkopta maalum iliyoleta kikombe cha ubingwa kwenye uwanja huo, benki hiyo iliandaa hafla kubwa ya kukabidhi ubingwa huo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wahudhuriaji wa tukio hilo ikiwemo usajili wa uanachama kwa mashabiki wa timu ya Yanga waliofika kwenye uwanja huo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter Nalitolela (Kulia) wakijipongeza kwa kufanikisha hafla hiyo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...