Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Katika kuelekea kilele cha Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari ambayo huadhimishwa May 3 kila mwaka Duniani suala la akili mnemba limeendelea kujadiliwa kwa upana kwa faida na hasara zake ambapo moja ya faida zake imeelezwa kuwa ni kuleta utambuzi wa mbolea gani inaweza kufaa katika eneo lipi hapa Nchini ili badala ya kuwa mbolea aina moja hivyo itaweza kutambua na kuwa nambolea tofauti tofauti.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanzilishi wa NGO's ya Omuka Hub Neema Lugangira katika moja ya mijadala iliyokuwa ikiendelea katika shamla shamla za kuelekea Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani inayofanyika Jijini Dodoma.

"Tunapoongelea akili mnemba kuna faida nyingi sana hakuna ambaye anaweza kupinga kwamba ina faida sana, tukichukulia mfano katika Sekta ya kilimo kwa kutumia akili mnemba tunaweza tukatambua labda ni mbolea gani ainaweza kufaa eneo gani la nchi ili badala ya kununua aina moja ya mbolea ambazo tunanunua kulingana na maeneo husikahiyi ni moja ya faida. Lakini hata katika Sekta ya Afya kuna faida zake,hata kwa wanafunzi kufanya tafita zao"

Sambamba na hayo pia Neema amaeleza Changamoto za hiyo akili mnemba kuwa ni pamoja na utoaji wa taarifa zisizo sahihi yaani upotoshaji wa Taarifa na kutoa mfano kilichotokea kwa Raisi wa Zambia mwaka ambapo clip ilisambaa ikisema kuwa Raisi huyo hatagombea tena Uraisi na vyombo vya habari vikaamini hivyo mpaka pale Ofisi ya Raisi ilipokanusha kuwa clip hiyo haina ukweli.

"Lakini pia kila lililo jema lina upande wake mwingine akili mnemba inachangamoto zake nyingi sana na changamoto hizi zisipotiliwa mkazo au maanani hata zile faida zitakuwa hazina maana".

"Katika changamoto zilizopo moja ni upotoshaji wa wa taarifa,Mfano mwaka jana Raisi wa Zambia ilitoka Video Clip yake ikisema kuwa yeye hatogombea tena Uraisi ilikuwa video ambayo ukiitizama unaona yeye kasema,ikaoneshwa kila mahali na hata vyombo vikubwa wakaichukua na kuiweka, lakini baadae Ofisi ya Raisi waksema si kweli na kuwa imetengenezwa sasa fikiria taharuki iliyokuwa imetokea hapo".

Pia amezungumzia masuala ya ukatili kwa wanawake na akili mnemba hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Hata Uchaguzi Mkuu wa 2025 kuwa waathirika wakubwa watakuwa ni Wanawake katika Siasa.


"Na hivi tunavyoelekea kwenye Uchaguzi nadhani kuna umuhimu mkubwa sana wa Wanahabari kabla ya habari kutoka,kuichapisha na kuisambaza kuhakikisha kwamba hii habari ni kwelie. Kwasababu inaweza kuzua taharuki kubwa sana".

"Lakini ukija katika eneo lingine ni kwenye ukatili wa kijinsia wa wanawake hasa linapokuja suala la matumizi ya teknolojia kwa bahati mbaya sana kati ya waathirika wakubwa ni sisi wanawake katika Siasa,kwani sisi soye sauti zetu zinajulikana video clip zetu zipo kwahiyo mtu anaweza akachukua maneno utafikiri wewe ndo umeyasema kumbe hujawahi kusema. Lakini mbaya zaidi uanweza ukatengenezewa kitu cha ajabu kwamba uko na mtu fulani na mkifanya jambo fulani na Uchaguzi ndo katikati umewaka moto,sasa kwa jambo hilo kwenye Uchaguzi itakuwaje,kwahiyo kunwa mambo lazima kayaangalia mapema".

Naye Harold Sungusia wakati akichangia Mada hiyo ya matumizi ya akili mnemba amesema kuwa katika changamoto hizo tusikate tamaa kwani anaamini pamoja na changamoto kuonekana kuwa nyingi lakini tukijipanga tunaweza fanya vizuri katika eneo hilo.

"Kitu ambacho nilikuwa najaribu kupendekeza kwenye hizi changamoto ni tusikate tamaa,lakini naamini kwamba tukijipanga vizuri bado tukafanya vizuri,kwasbabu tayari tunao Watanzania wanaofanya vizuri.Mfano kwenye Sekta ya afya,Sekta imetoa muongozo wa matumizi ya akili mnemba katika sekta afya Nchini na Imeonesha kusapoti vijana na vikundi mbalimbali kubadili matuzimi mabaya ya akili bandia na kuwa matumizi mazuri".

Kwa upande wake Nuzulack Dausen ambaye ni Mtendaji Mkuu Nukta Afrika amesema kuwa akili mnemba katika sekta ya habari inatumika katika uchakataji wa habari yani kuanzia kukusanya habari hizo,tofauti na zamani kulikuwa hakuna hiko kitu.

"Kwenye sekta hii ya habari akili mnemba inatumika katika mfumo wa uchakataji wa habari kwamba kuanzia kukusanya habari,zamani tulikuwa tulitumia maiki na kwenda kuchakata Radioni lakini saizi tunaweza kutumia akili mnemba kufanya hicho kitu".





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...