Hatifungani ya kijani ya Mamlaka ya Maji Tanga ambayo ni ya Kwanza kuwahi kutokea Afrika Mashariki imefanikiwa kukusanya asilimia 103% ya mauzo yaliyotarajiwa.
Hatifungani hiyo yenye thamani ya shilingi Bilioni 53.12 ilianza kuuzwa tarehe 22, Februari 2024 na kufanikiwa kuorodheshwa kwenye soko la hisa Dar es salaam (DSE) leo tarehe 15 Mei,2024
Hatifungani hiyo yenye thamani ya shilingi Bilioni 53.12 ilianza kuuzwa tarehe 22, Februari 2024 na kufanikiwa kuorodheshwa kwenye soko la hisa Dar es salaam (DSE) leo tarehe 15 Mei,2024
Tanga UWASA imeweza kuwavutia wawekezaji wa Kimataifa ambapo asilimia 35 ya makusanyo ni kutoka kwa wawekezaji wa nje na asilimia 65 ni wawekezaji wa ndani
Hatifungani hii sasa itauzwa na fedha zitakazopatikana zitagharamia miundombinu endelevu ya usambazaji maji na uhifadhi wa Mazingira Tanga.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mwigilu Nchemba wakati akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa hafla hiyo leo Mei 15,2024 katika Ukumbi wa Kambarage jijini Dodoma
"Tukio hili na matukio mengine ya aina hii ambayo yamefanyika katika Siku za karibuni kwa taasisi na makampuni binafsi ni ushahidi wa wazi kuwa Mkakati wa Serikali wa kugharamia miradi ya Maendeleo kwa njia mbadala uliozinduliwa Mwezi Mei,2021 unatekelezeka pia kwa taasisi za Umma"amesema
Ameongeza kuwa kwa kuzingatia kuwa fedha zilizohitajika kwa utekelezaji wa mradi huo zimepatikana zote Wizara ya Fedha itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mafanikio ya mradi huo kama ilivyopangwa.
Naye Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesisitiza kuwa mahitaji ya kifedha kwa ajili ya miundombinu ya Maji nchini kote bado yako juu sana.
"Wingi wa vipaumbele vya maji na ufinyu wa bajeti husababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi, upatikanaji wa fedha kupitia hatifungani kama hii ya Tanga inasaidia juhudi za serikali na kuharakisha utoaji wa huduma bora ya maji Kwa wananchi, amesema
Aidha Aweso ametoa rai kwa Mamlaka nyingine za Maji kujifunza kupitia hatifungani ya Tanga UWASA na kuiga mfano huo.
Katika salaam zake,Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji Tanzania (UNCDF) Peter Malika ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ubunifu na kufanikiwa kukamilisha tukio hilo la kihistoria kwa Tanga UWASA.
"Kwa kushirikiana na Serikali umuhimu wa msaada wetu kama taasisi ya fedha ya Maendeleo umesababisha kuondoa na kufafanua vizwako vya kitaalam na kisera walivyokuwepo kabla ya kutolewa hatifungani hii"amesema
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na dhamana (CMSA) Nikodemus Mkama amesema kuwa mafanikio ya utoaji na kuorodheshwa kwa hatifungani ya Tanga UWASA kwenye soko la hisa Dar es salaam unaimarisha nafasi ya Masoko ya Mitaji ya Tanzania kwenye ramani ya masoko ya Mitaji ulimwenguni.
Naye Bi.Mary Mnaiwasa Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la DSE ameeleza kuwa kuorodheshwa kwa hatifungani ya Tanga UWASA kunadhihirisha nguvu ya Ushirikiano Kati ya sekta ya Umma na binafsi,pamoja na adhma ya wadau kufanya uwekezaji ambao unazalisha faida.
"Soko la hisa la Dar es salaam linapenda kuzialika taasisi za Umma, Makampuni na taasisi binafsi kuendelea kutumia njia hii kuongeza Mitaji yenye lengo la kuchagiza na Kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla"amesema
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA Mhandisi Geofrey Hilly amesema kuwa ni fahari kubwa kushuhudia mafanikio ya kuorodheshwa kwa hatifungani hiyo ya kijani.
Pia amesisitiza umuhimu na malengo yake katika kuendeleza miundombinu endelevu ya Maji na uhifadhi wa Mazingira,huku akitoa shukurani kwa wawekezaji wote, Serikali,washirika na wadau mbalimbali kwa Ushirikiano wao.
Wadaa wengine Muhimu waliohusika na uandaaji wa hatifungani hii ni pamoja na Benki ya NBC Mshauri mwelekezi,FSD Afrika Upatikanaji wa hati ya kijani FIMCO na Global Sovereign Advisory Fedha na Uwekezaji,ALN Tanzania Sheri Innovex Uhasibu. (Imeandikwa na Manase Madelemu)
Picha mbalimbali kwenye hafla ya ufunguzi wa hatifungani ya kijani ya Mamlaka ya Maji Tanga ambayo imefanyika leo Mei 15,2024 katika Ukumbi wa Kambarage jijini Dodoma (Picha na Manase Madelemu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...