Mstahiki Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilemela,Renatus Mulunga akifungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo leo.
Mchumi wa Manispaa ya Ilemela, Herbert Bilia,akitoa ufafanuzi na kujibu maswali ya baadhi ya madiwani wa manispaa hiyo leo.
Diwani wa Nyam'hongolo, Andrew Nginila akiuliza maswali katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo, leo wakati wa maswali ya papo kwa hapo.
Picha zote na Baltazar Mashaka


NA BALTAZAR MASHAKA,ILEMELA
MANISPAA ya Ilemela tangu Janauri hadi Machi 31, mwaka huu,imekusanya zaidi ya sh.bilioni 10 sawa na asilimia 68 ya maksio ya bajeti ya mapato ya ndani ya mwaka wa fedha wa 2023/24.

Pia,katika kipindi hicho cha robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha halmashauri hiyo imetekeleza miradi ya zaidi ya sh.bilioni 3.9 kutoka Serikali Kuu ikiwemo miradi ya TASAF na TACTIC.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Marco Isack amelieleza Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,leo kuwa katika kipindi cha robo ya tatu ( Januari hadi Machi) mwaka wa fedha wa 2023/24.

Amesema tangu Januari manispaa hiyo imekusanya sh.bilioni 10.1 za makisio ya bajeti ya mapato ya ndani sawa na asilimia 68 ambapo katika robo tatu ya mwaka 20223/24 imetekeleza miradi ya maendeleo ya TACTIC na TASAF yenye thamani ya sh. bilioni 3.9 zilizotolewa na serikali kuu.

“Miradi ya TASAF yenye jumla ya sh. milioni 376.5 kati ya sh.milioni 196.6 zimetumika kujenga bweni la wasichana la Shule ya Sekondari Kayenze,zaidi ya milioni 179 za ujenzi wa bweni la wasichana wa Shule ya Sekondari Buswelu,”amesema Isack.

Amesema halmashauri hiyo inatekeleza mradi wa TACTIC wa ujenzi wa barabara ya Buswelu-Busenga-Cocacola ya urefu wa km 3.3 na barabara ya Buswelu –Nyamadoke-Nyamh’ongolo km 9.5 na mkandarasi amelipwa sh.bilioni 3.5 ambapo mradi huo umefikia asilimia 12.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema mapato ya ndani katika robo ya tatu sh.milioni 679.3 zilielekezwa katika miradi ya maendeleo mbalimbali katika kata za halmashauri hiyo ikiwemo milioni 170 za malipo ya mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya urefu wa km 13 kutoka Hospitali ya Wilaya ya Ilemela hadi Ilalila.

Pia, sh.milioni 167.3 za asilimia 10 ya mapato ya ndani zilipelekwa katika mfuko wa uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake,vijana na walemavu,sh.milioni 164.2 za fidia ya ardhi katika maeneo mbalimbali miradi ikiwemo Buswelu–Nyamadoke-Nyamh’ongolo,Buswelu-Busenga-Cocacola sh.milioni 12.5 za fidia kwa wananchi wanne (4).

Kwa mujibu wa Isack maeneo mengine ambayo fedha za fidia ya sh. milioni 16.3 zilielekezwa ni mitaa ya Nyafula,Sangabuye na Lugeye kwa wananchi watano,eneo la viwanda Nyamh'ongolo sh. milioni 48 kwa wananchi wawili na eneo la Nyamanoro sekondari zaidi ya milioni 25 kwa mwananchi mmoja.

Pia, sh.milioni 48.02 za fidia ya ardhi kwa wananchi wanne waliokuwa wakimiliki baadhi ya maeneo ya Lumala sekondari na Shule ya Msingi Mwambani,Ibinza Nyamh'ongolo sh.milioni 2.8 ( mwananchi mmoja),Shibula milioni 2 (mwananchi mmoja),Pasiansi milioni 3(mwananchi mmoja), na sh. milioni 49.9 za wananchi wanne waliokuwa wakimiliki eneo la East Buswelu.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema sh.milioni 41.1 zilitumika kujenga matundu 10 ya vyoo na mabafu matatu,katika mialo ya Mihama,Igombe,Kabangaja na ujenzi wa ofisi ya Mwalo wa Mihama huku mashine (POS) mpya 50 za kukusanyia mapato zikigharimu zaidi ya milioni 34.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga amesema kuwa maendeleo hayawezi kunyesha mitihili ya mvua bali yanatafutwa,hivyo amewasistiza madiwani wasimamie ukusanyaji wa mapato wakishirikiana na wakusanyaji,zipatikane fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Diwani wa Nyakato (CCM),Jonathan Mkumba ameshauria wataalamu wa Idara ya Ardhi kushusha chini katika kata kliniki ya ardhi kusuluhisha na kutatua kero ya migogoro ya ardhi.
“Ardhi inagusa maisha ya watu,migogoro ya ardhi ni kitanzi tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Kiliniki ya ardhi imesaidia kupunguza migogoro,hivyo ishushwe chini maana wananchi wamechoka kuja halmashauri watumishi wa idara hiyo watenge siku katika kata kuwasikiliza wananchi,”amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...