Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiondoa kitambaa tayari kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Na Alex Sonna-KASULU VIJIJINI
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limeanza kutekeleza agizo la Serikali la matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kufunga mitungi katika vikosi vyake lengo likiwa ni kutunza na kulinda mazingira.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema hayo mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Brigedia Jenerali Mabena amesema katika kutekeleza kwa vitendo agizo la hilo,JKT kwa kushirikiana na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) walizunguka katika vikosi vyote vya JKT nchini ili kuangalia namna bora ya kuweka miundombinu.

Amesema vikosi vingine vinaendelea kutengeneza miundombinu kama ilivyokuwa imeshauriwa na ile kamati ambayo imehusisha REA na wataalamu kutoka JKT.

"Sasa kwa kuwa wapo na wanaendelea ile kamati maalum waliweza kupita kwenye vikosi vyote na kuweza kuangalia miundombinu na kutoa maelekezo na ushauri namna ya kufanya.

"Ni pamoja na kuandaa majiko na kusimika mitungi mikubwa ya gesi huku wakiendelea kusubiri Mpango wa REA ili kuhakikisha mazingira yanakuwa salama,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
Amesema kikosi cha 825 Mtabila na chenyewe kipo katika hatua za utekelezaji.

Brigedia Jenerali Mabena amekipongeza kikosi hicho kwa hatua hiyo ambayo wameifanya kwani ni maagizo ya Serikali na kuwa wadau wa matumizi ya kupikia.

Amesema JKT wanawahudumia wadau wengi kwani vikosi vya kujenga Taifa kwa mwaka mmoja wanakuwa na vijana wa kwa mujibu wa sheria wanaofikia laki moja.

"Utaona vijana hawa wanahitaji kupata chakula kwa kuwa JKT sisi ni wadau wakubwa na mazingira yetu yanaendelea kuwa salama tunayalinda kwa namna yoyote.

"Na katika kuyalinda kwanza kabisa hatukati miti na tumekuja na kampeni kabambe ya tunapanda miti katika maeneo yetu ya vikosi lakini kwa kutumia nguvu kazi kwa kupanda katika Wilaya na Halmashauri zinazotuzunguka kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani,"amesema Mkuu huyo wa tawi JKT

Kwa upande wake Kamanda Kikosi 825 KJ, Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya,amesema zoezi hilo lilianzia mara baada ya maelekezo ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Ofisi ya Muungano na Mazingira kupitia Makao Makuu ya JKT

Amesema wao kama kikosi walipokea maelekezo hayo na kwa sababu wanawahudumia watu wengi na wao waliamua kulitekeleza.
"Hili jiko la gesi tumetumia gharama zote kwa vyanzo vya ndani.Lakini pia ni sehemu kama shamba darasa kujifunza na jinsi ya kutunza mazingira,"amesema

Amesema kama kikosi wanaendelea na jitihada za kupanda miti ambapo mpaka sasa wamepanda miti 13,000 na 1000 ya matunda.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiondoa kitambaa tayari kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akisoma ujumbe mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiangalia majiko na Mitungi mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Kamanda Kikosi 825 KJ, Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa jiko la gesi katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...