Nani alishawahi kufikiria kwamba itafika siku ambayo vile unavyolinda simu yako dhidi ya uhalifu wa mtandaoni ndivyo itakavyokuja kuwa sawa na kwa luninga yako?

 

Ndiyo, luninga yako nayo inahitaji ulinzi wa taarifa zako za siri, kama ulikuwa haufahamu au hautilii maanani basi leo utajifunza kitu.

 

Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yamepelekea mwingiliano wa vifaa tofauti vya kidigitali vinavyounganishwa na mtandao wa intaneti. Kwa mfano, sasa mtu anaweza kusimamia na kufuatilia mwenendo wa matumizi ya vifaa tofauti vya umeme nyumbani kwake kama vile luninga, mashine ya kufulia, na kiyoyozi mahali na muda wowote alipo.

 

Mwingiliano huu humlazimu mtumiaji wa vifaa kuweka taarifa zake za siri ili kuweza kuunganishwa navyo na hatimaye kuvisimamia kwa urahisi mahali popote alipo. Hivyo mtu hujikuta anaingiza taarifa zake binafsi kama vile majina, namba za simu, barua pepe, pamoja na nywila.

 

Bila shaka hii ni faida nyingine inayotokana na maendeleo ya teknolojia na mawasiliano. Lakini tunajilindaje dhidi ya hatari zinazokuja na mabadiliko haya? Watu wengi hudhani kwasababu luninga ni kifaa ambacho tunakitumia na kukiacha nyumbani au sehemu zetu kazi basi hakipo hatarini kushambuliwa na uhalifu wa mtandaoni.

 

Ukweli ni kwamba tunapaswa kuwa makini na uhakika wa usalama wa taarifa zetu binafsi katika vifaa vyote vya kiteknolojia na mawasiliano tunavyovitumia.

 

Kampuni ya Samsung kwa kuliona hilo mwaka 2013 ilitambulisha programu ya Knox kwa ajili ya kulinda mifumo ya uendeshaji na vifaa vyake vya kielekroniki.

 

Samsung Knox ni jukwaa la biashara la kupangilia na kudhibiti vifaa vya mkononi - ikileta ufanisi na kutoa matumizi mahususi katika sekta mbalimbali. Huifanya miundombinu ya vifaa vya mkononi ikiwa imeunganishwa, salama na yenye tija. 

 

Tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka kumi sasa, imefanikisha ulinzi wa vifaa vya Samsung takribani bilioni mbili na inatumika kusimamia vifaa zaidi ya milioni 150. Ikiwa inaaminiwa duniani kote, Knox imesaidia biashara zaidi ya 35,000 kufanikisha malengo yake kwenye mataifa tofauti.

 

Hivyo, ukiwa kama mtumiaji wa luninga za Samsung haupaswi tena kuwa na wasiwasi kuhusu taarifa zako binafsi ulizoziingiza ili kunufaika na huduma mbalimbali zinazotumia mtandao wa intaneti.

 

Samsung Knox hutambua kikamilifu matishio ya udukuzi yanavoweza kutokea kwa wakati halisi, ikiripoti mabadiliko yoyote ambayo hayajaidhinishwa. Inathibitisha kurasa tofauti za tovuti zinazofikiwa na watumiaji, ikizuia kwa hiari tovuti hatarishi ili kulinda taarifa binafsi za mtumiaji na faragha yake. Inahakikisha ulinzi thabiti wa taarifa binafsi za watumiaji kupitia muunganisho salama na Samsung Knox Vault, kichakataji mahususi kwa usalama.

 

Luninga za Samsung zinalindwa dhidi ya hatari za uhalifu wa mtandaoni kutokana na uwepo wa program ya Knox ambayo huifanya mifumo ya uendeshaji na kifaa kuwa salama.

 

Unaweza kuwa unajiuliza kwanini ni muhimu kutumia luninga inayozingatia usalama wa taarifa zako binafsi. Lakini kumbuka kwamba ujio wa luninga za kisasa umekuja na fursa ya matumizi ya huduma tofauti zilizounganishwa na intaneti kama vile majukwaa ya mpira, filamu, michezo, burudani na kuperuzi taarifa mbalimbali, ambazo kwa namna moja ama nyingine zinahitaji uingize taarifa zako binafsi.

 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...