Na Mwandishi Wetu,Dodoma
MADEREVA bodaboda 145 katika Jiji la Dodoma- wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani awamu ya pili yalioanza Aprili 15 Aprili na kukamilika Mei 4 mwaka huu.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Uswisi kwa kuahirikiana na Shirika la Amend Tanzania yamehitimishwa kwa madereva bodaboda hao kupatiwa vyeti vya ushiriki.
Akizungumza mbele ya madereva bodaboda pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani Naibu Meya wa Jiji la Dodoma aliyekuwa mgeni rasmi Asma Karama amewataka madereva hao kuwa mabalozi kwa bodaboda ambao hawajafikiwa na mafunzo hayo.
"Niwasihi madereva wote waliopokea mafunzo haya kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani katika maeneo yao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani,"amesema Naibu Meya Asma.
Awali Simon Kalolo ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania amesema katika utekelezaji wa mafunzo hayo Shirika la Amend linashirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, viongozi wa Serikali za mitaa na shirika la Msalaba Mwekundu wakati wa kutoa mafunzo hayo.
Pia amesema kuwa kupitia mradi huo hadi sasa, mradi huu wa usalama barabarani kwa vijana umewafikia madereva wa pikipiki 398 jijini Dodoma.
"Madereva waliohudhuria mafunzo haya wamepatiwa vyeti vya ushiriki pamoja na viakisi mwanga vyenye ujumbe wa usalama barabarani.Awamu ya kwanza ya mafunzo haya, madereva 253 kutoka kata za Jiji la Dodoma wamenufaika."
"Katika utekelezaji wa mafunzo haya, shirika la Amend linashirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, viongozi wa serikali za mitaa na shirika la Msalaba Mwekundu, linalowapatia madereva elimu muhimu ya huduma ya kwanza.
"Tunayofuraha tunapohitimisha awamu ya pili ya mafunzo haya hapa Dodoma, kuna mabadiliko makubwa kwani madereva wengi waliopatiwa mafunzo haya wanafahamu Sheria za usalama barabarani pamoja na alama zilizopo Kwetu hili tunasema ni hatua kubwa ya kusaidia kupunguza ajali kwa kundi hili,"amesema Kalolo.
Ameongeza kuwa katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, madereva 253 kutoka katika Kata mbalimbali za Jiji la Dodoma zikiwemo Kata ya Uhuru ambako mafunzo haya yamekuwa yakifanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...