Magari ya Mizigo, Mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama kwa siku sita katika barabara ya Lindi-Dar es Salaam eneo la njia nne (Mikereng’ende) hadi Somanga yakitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam yaanza kuruhusiwa kuendelea na safari.

Hatua hiyo imechukuliwa leo asubuhi, tarehe 09 Mei, 2024 Mkoani Lindi mara baada ya kukamilisha urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo ya Mikereng’ende, Songas na Somanga ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Akisimamia zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amewataka wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara kusafiri kwa tahadhari ambapo maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.

“Naipongeza Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zilizofanyika ndani ya muda mchache na leo tunashuhudia magari yaliyokwama yameruhusiwa kuendelea na safari”, Amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, Kazi ya urejeshaji wa miundombini ya barabara ya Lindi - Dar es Salaam eneo la Nangurukuru ipo katika hatua ya ukamilishaji chini ya usimamizi wa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara (TANROADS)

Kwa upande wa wananchi, Wameishukuru Serikali kwa namna ambavyo wamerejesha mawasiliano ya barabara kwa vipande hivyo na kuweza kuruhusiwa leo baada ya siku sita kukwama katika barabara hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...