Na Stephano Mango, Mbinga

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Desderius Haule amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga itaendelea kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ukamilishaji na utekelezaji wa miradi mipya itayokwenda kuleta tija kwa wananchi.

Haule amebainisha jana akijibu swali la Diwani wa Viti maalum Kata ya Kihangimahuka Leonora Mwinuka katika mkutano wa baraza la madiwani kujadili taarifa za robo ya tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2024 lililouliza Je Halmashauri ina mkakati gani wa kukamilisha miradi viporo.

Haule ameeleza kuwa pamoja na shughuli nyingine utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni kipaumbele cha Halmashauri katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza hilo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Rwiza ametoa rai kwa madiwani kushirikiana na wataalam wa Halmashauri katika kukusanya mapato ili fedha hizo zitumike katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Rwiza amebainisha kuwa pamoja na vyanzo vya mapato vilivyopo,Halmashauri inaendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato pamoja na kuondokana na utegemezi wa fedha kutoka Serikali Kuu pekee.

Akitoa salamu za Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori amempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuvuka lengo la makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akichangia mada katika Mkutano huo Diwani wa Kata ya Matiri Mhe. William Mbwambo ametoa rai kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kuona namna bora ya kuwafikia wanawake wengi zaidi wakati wa zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...