NA WILLIUM PAUL, SAME.
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewataka wananchi kwenye maeneo yote yenye mgogoro wa mipaka katika vijiji vinne vya Bangalala, Makanya, Nasulo na Mwembe kutoendelea na shughuli yeyote mpaka hapo mwezi June mwaka huu Serikali itakapotoa ufumbuzi wa mgogoro huo.
Mkuu huyo wa Wilaya amezungumza hayo kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Bangalala wenye lengo la kuwaeleza wananchi mchakato unaoendelea juu ya ahadi ya Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi hao kuhusu utatuzi wa mgogoro huo.
Aidha Kasilda alisema kuwa amefurahishwa na kauli ya Waziri Silaa akiwa bungeni ambapo amesema mapema baada ya kumaliza vikao vya Bunge mwezi June anakuja kuleta majibu ya mgogoro huo na kuwaomba wananchi kuwa na uvumilivu.
Awali kwenye mkutano huo wananchi wamemueleza Mkuu wa Wilaya juu ya sintofahamu miongoni mwao kinachoendelea baada ya Waziri wa Ardhi Jerry Silaa kuahidi wananchi hao kuwa mwezi Machi mwaka huu atakuwa tayari amemaliza mgogoro huo.
Hata hivyo kutokana na Waziri Silaa kubanwa na majukumu akiwa bungeni kwenye vikao vya bajeti vinavyoendelea amelezima kuwatoa hofu wananchi hao kuwa mapema baada ya kumaliza majukumu hayo mwezi June mwaka huu anakuja kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka 19.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...