Na Mary Margwe, Simanjiro

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Fakii Raphael Lulandala amesema suala ya kuwepo kwa huduma ya  Zahanati na maji ndani ya Machimbo ya Tanzanite katika Mji Mdogo wa Mirerani ni jambo linalotakiwa kutekelezwa Kwa haraka zaidi kutokana na Msongamano wa wingi wa watu ndani ya Ukuta huo wa Magufuli.

Hayo amesema juzi alipokua kwenye ziara ya kutembelea baadhi ya Migodi kama Mgodi wa " Kitalu C" wa Kampuni ya  Flanone mining and Gems Ltd Chini ya Mkurugenzi wake Onesmo Anderson Mbise na Francis Matunda, Mgodi wa Gems & Rock chini ya Mkurugenzi wake Joel Saitoti, Mgodi wa Bilionea Saniniu Laizer na Mgodi wa Kilimanjaro Mining.

Lulandala amesema ni vigumu kusukuma na kusimamia usichokifahamu ama kukijua, hivyo kufika kwake na kutembelea baadhi ya Migodi hiyo ameweza kufahamu baadhi ya changamoto muhimu na kubwa zinazotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka iwezekanavyo ili wananchi waweze kupata huduma za afya na Maji kiurahisi.

" Nilichokifanya leo ni kupita maeneo mbalimbali ndani ya Machimbo ya Madini ya Tanzanite katika Mji huu mdogo wa Mirerani kuanzia Ofisini kwa Afisa Madini Mkazi Mirerani ( RMO) Chacha Marwa Nchagwa, na kwenye maeneo yetu yote ya Kimkakati na ya Usalama, na ya kiuangalizi yanayohusiana na eneo letu la Migodi " amesema Lulandala.

Aidha amesema akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Afisa Madini Mkazi Mirerani RMO Chacha Marwa Nchagwa wamepita kwenye maeneo Mengine ya kawaida ya kijamii kwasababu Kuna shughuli nyingi zinaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ndani ya Mji Mdogo wa Mirerani.

" Nafahamu kwamba kuna huduma za kijamii ndani ya Mgodi , na wakati mwingine ninakua nikipita naambiwa pia Kuna mahitaji humu ndani ya na huduma zingine za afya, Sasa ni vigumu kusukuma na kusimamia usichokifahamu ama kukijua Kwa uhakika kama huko ndani kukoje, Kuna watu kiasi gani, wanaishije, na wanafanya nini, kwahiyo tukaona ni vizuri tupite tujifunze, Sijapita kwa maana ya kusema leo nasikiliza kero, lakini nitakua na utaratibu wa mara moja moja na wenzangu kwaajili ya kuja kusikiliza kero na kupokea Ushauri" amesema Mkuu huyo.

Amesema ni vema wananchi wakaamini kuwa Serikali yao ya awamu ya sita inavyofanya kazi chini ya Jemedali Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya kazi usiku na mchana Kwa lengo la kuharakisha Maendeleo ya Watanzania huku ikifahamu mchango mkubwa unaofanywa na wachimbaji wadogo wa Madini watokao katika Mji Mdogo wa Mirerani, hivyo ni vema wakafanya kazi kikamilifu ili kuweza kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuondokana na umaskini.

" Mimi ni Mkuu wenu wa Wilaya hii ya Simanjiro, maana yake tupo hapa kumuwakilisha Mh.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa niaba yake na ninyi wote na shughuli zenu mbalimbali ni wapiga kura wake, kwahiyo sisi tunawahibika kufika kwenu kuwasililiza, lakini hata kuona namna mnavyoishi , zipo changamoto zingine tumejionea tulivyokua tunapita kuja huku kama za barabara lakini nimegundua kwamba kumbe ni kweli huku ndani Kuna uhitaji mkubwa wa huduma za kiusalama nansinza kiusalama pekee hata za afya" amesema Lulandala.

" Tayari tumeshapata maelezo kibajeti humu ndani Kuna suala la Zahanati na Maji ndani ya Ukuta , ni katika vitu tutasimamia kikamilifu kwasababu tumeona , hasa kwenye maeneo Maalum yenye Msongamano wa watu " ameongeza Mh. Lulandala.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...