Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WASOMI wa kada mbalimbali pamoja na wabobezi wa masuala ya ulinzi, Usalama pamoja na Diplomasia katika Bara la Afrika wameelezea mambo muhimu yanayoweza kusaidia katika harakati za kuimarisha amani katika Bara hilo yakiwemo ya kuwashirikisha vijana.
Wakizungumza katika Kongamano maalumu lililoandaliwa na Uongozi Institute kujadili masuala ya ulinzi na Usalama Afrika,wasomi na wabobezi wa ulinzi na amani wamesisitiza uongozi bora, taasisi imara na uwezeshaji wananchi kiuchumi ni miongoni mwa mambo ya msingi katika ulinzi wa amani na usalama wa Afrika.
Akizungumza katika Kongamano hilo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Ulinzi na Usalama wa Umoja wa Afrika (AU), Balozi Bankole Adeoye amesema kuna haja Baraza la Usalama la Afrika kuwashirikisha vijana.
"Nani anapaswa kuwa kiongozi, nani anapaswa kushauri, nani anapaswa kuwa mfano wa amani Afrika lakini tuwe na taasisi imara hapo tutakuwa na amani tunayoitaka Afrika," amesema.
Ameongeza kwamba amani inayotakiwa Afrika ni ile itakayowezesha vijana na wanawake kuwezeshwa kwa kila namna huku akisisitiza amani hiyo itajengwa kwa kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto Afrika.
Kwa upande wake Balozi mstaafu wa Tanzania, Brigedia Jenerali mstaafu Paul Mella amefafanua kuwa hivi sasa mahitaji vya ulinzi wa usalama yanaongezeka kwani machafuko ya nchi moja na nyingine yanaongezeka pia.
Amesema changamoto kubwa ni maeneo mengi wanakotumwa walinzi wa amani huwa ni makubwa kuliko vikosi vinavyotumwa na baadhi ya nchi, pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa, lakini kuna changamoto ya kuyafikia maeneo mbalimbali.
Hata hivyo amesema jukumu la kulinda amani na kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa salama ni jukumu la kila mmoja wetu na sio vyombo vya ulinzi na Usalama pekee huku akitoa mifano kuwa katika maeneo ambayo kumekuwa na changamoto za kiusalama kumekuwepo na taasisi mbalimbali ambazo zote zinashiriki katika kulinda masuala ya ulinzi na usalama.
Wakati huo huo Mhadhiri wa Masomo ya Kimkakati katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Profesa Eginald Mihanjo ameongeza kwamba ulinzi na amani kinashabihiana na uwezo wa kiuchumi wa wananchi.
Amesisitiza kwamba kuwa, msingi wa uchumi ni wananchi hasa vijana baada ya kuhitimu elimu ya juu wawe katika ajira,hivyo amesema ni vigumu nchi husika kuwa na amani kwa kuwa vijana wengi hawana cha kufanya.
"Kufikia mwaka 2050 zaidi ya asilimia 50 ya watu wa Afrika watakuwa vijana na inawezekanaje kuwa na amani iwapo wanataka kuingia kusaka fedha na hawana ajira," ameeleza.
Pamoa na hayo Baraza la Usalama la Afrika limetimiza miaka 20,hivyo wasomi hao wameeleza iko haja kwa Bara hilo kuhakikisha kinaendelea kuweka mikakati itakayoshirikisha makundi yote yakiwemo ya vijana kwani takwimu zinaonesha mwaka 2050 nusu ya watu wa Afrika watakuwa chini ya miaka 25.
"Kufikia mwaka 2050 zaidi ya asilimia 50 ya watu wa Afrika watakuwa vijana na inawezekanaje kuwa na amani iwapo wanataka kuingia kusaka fedha na hawana ajira," ameeleza.
Pamoa na hayo Baraza la Usalama la Afrika limetimiza miaka 20,hivyo wasomi hao wameeleza iko haja kwa Bara hilo kuhakikisha kinaendelea kuweka mikakati itakayoshirikisha makundi yote yakiwemo ya vijana kwani takwimu zinaonesha mwaka 2050 nusu ya watu wa Afrika watakuwa chini ya miaka 25.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...