*Yataka waombaji kuweka taarifa sahihi kuepusha usumbufu

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Tanga ,
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) imefungua dirisha la Udahili kwa Wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kwa ngazi ya Astashada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na Baraza hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea Mjini Tanga Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Adolf Rutayuga amesema dirisha hilo limefunguliwa rasmi Mei 27 mwaka huu ikiwa ni fursa katika Maonesho hayo wakaanza kuomba kutokana na uwepo ushiriki wa Vyuo vyote katika Maonesho.

Dkt.Rutayuga amesema kuwa maombi ya udahili kwa kozi ambazo si za Afya na Sayansi Shirikishi na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zitolewazo katika Vyuo Vya Zanzibar yatumwe moja kwa moja kwenye Vyuo husika kuanzia Mei 27 hadi Julai 14 mwaka huu kwa awamu ya kwanza.

Hata hivyo amesema maombi ya kozi za Afya na Sayansi Shirikishi kwa upande wa Tanzania Bara yatafanyika kupitia mfumo wa udahili wa pamoja (CAS) unaopatikana katika tovuti ya Baraza www.nactvet.go.tz kuanzia Mei 27 hadi Juni 30 mwaka huu kwa awamu ya kwanza.

Aidha Dkt.Rutayuga amesema kuwa zinazoombwa na vyuo vinavyotoa kozi hizo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Muongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2024/2025 ambao Muongozo huo unapatikana kwenye tovuti ya www.nactvet.go.tz.

Dkt.Rutayuga amewataka waombaji wote kuandika taarifa zao kwa usahihi na umakini pamoja na kutunza kumbukumbu watazopatiwa na Baraza bila kumpatia mtu mwingine yeyote ili kuepusha usumbufu katika zoezi zima la maombi ya kujiunga na kozi kwenye vyuo mbalimbali.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga akizungumza na Waandishi habari (hawapo) pichani kuhusiana na kufunguliwa kwa dirisha la udahili wa kujiunga na Astashada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...