Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Shirika la nyumba la Taifa Mkoa wa Dodoma katika mafanikio yake ya miaka 3 ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan limejivunia kuanza kutekeleza Mpango wa ujenzi wa Nyumba 5000 za gharama ya kati ujulikanqo kama Samia Housing Scheme ambapo Dodoma zitajengwa nyumba 100 katika eneo la Medelii.

Taarifa hiyo ameitoa na Gibson Mwaigomole ambaye ni Meneje wa Shirika la Nyumba Taifa kwa Mkoa wa Dodoma ameeleza hayo .apema leo hii May 22,2024 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafaniko ya Shirika hili kwa kipindi cha miaka ya Uongozi wa Dkt Samia.

"Shirika limeanza kutekeleza Mpango wa ujenzi wa nyumba 5000 za gharama ya kati ujulikanao kama Samia Housing Scheme (SHS) ,na kwa Mkoa wa Dodoma Shirika linatarajia kujenga nyumba 100 katika eneo la Medelii".

Aidha Bwana Mwaigomole ameongeza kuwa wana miradi miwili ya ushauri elekezi ambayo hii ni miradi ya nje na wanafanya kama washauri waelekezi ambayo ni ya Wizara ya Fedha na Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazinira ambayo thamani yake ni Shilingi 6,834,683,333.33. Ambapo ujenzi wa umefikia asilimia 65.2 kwa Wizara ya fedha na asilimia 75 kwa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira.

"Tuna miradi miwili ya Ushauri elekezi hii ni miradi ya nje ambayo tunafanya kama washauri elekezi amabyo ni Wizara ya fedha pamoja na Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira. Gharama ya ushauri elekezi kwa miradi hii kwa ujumla wake ina thamani ya kiasi cha Shilingi 6,834,963,333.33. Wizara ya fedha ujenzi umefikia asilimia 65.2 na ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira ujenzi umefikia asilimia 75".

Pia NHC imefanya ujenzi wa Ofisi wa Wizara nane ambayo pa nayo ni miradi ya nje ambayo wanafanya kama Wakandarasi ambayo ni pamoja na Wazaira ya Ardhi,Nishati,Madini,Mawasiliano, Mifugo,Viwanda,Mambo ya Ndani na Wizara ya Utamaduni ambapo gharama ya miradi hii ni Shilingi 186,833,463,553.8. Na ujenzi umefikia asilimia 82.

"Pia tuna ujenzi wa Wizara nane,hii ni miradi ya nje ambayo tunafanya kama Wakandarasi ambayo ni Wizara ya Ardhi,Nishati, Madini,Mawasiliano, Mifugo,Viwanda,Mambo ya Ndani na Wizara ya Utamaduni. Gharama ya miradi hii kwa ujumla wake ina thamani ya kiasi cha Shilingi 186,833,463,553.8. Maendeleo ya ujenzi wa miradi hii ki wastani kwa sasa yamefikia 82%".

Sambamba na hayo pia amesema kuwa katika miaka mitatu hiyo Shirika limefanya ukarabati mdogo na mkubwa katika nyumba zake za kupangisha ambazo zipo katika Jiji la Dodoma maeneo ya Mpwapwa,Kiwanga Iringa Road.

"Katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Shirika limefanya ukarabati mdogo na mkubwa katika nyumba zake za kupangisha ambazo zipo katika Jiji la Dodoma. Shirika limefanya ukarabati mkubwa wa kupaka rangi katika majengo yaliyopo kiwanja 2/F Old Mpwapwa Flats na Kiwanga 17,18,19 &20/× Iringa Rd Flats".

Shirika limekamilisha mradi wa wenye thamani ya milioni 700 ambao ni ujenzi wa jengo la Wakala wa Ununuzi wa Serikali (GPSA) katika eneo la Mtumba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...