Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania kufuatia Kifo cha Rais wa Nchi hiyo Hayati Ebrahim Raisi kilichotokana na ajali ya Helikopta nchini Iran. Rais Samia alisaini Kitabu hicho katika Ubalozi wa Iran uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024. Kushoto ni Balozi wa Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh pamoja na Maafisa Mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Nchi hiyo uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2024

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...