Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ametembelea na kukagua utoaji huduma katika zahanati ya kijiji cha Leremeta ambapo amehoji kuhusu umeme unaopatikana katika zahanati ili kujua unawezesha mitambo yote kufanya kazi ipasavyo.


Katika majibu yake, uongozi wa zahanati hiyo umesema kuwa umeme hauridhishi kwakuwa ni single phase na moto unaopatikana ni mdogo hali inayopelekea hata kipimo kidogo cha damu kutoweza kufanya kazi.

Naye, Meneja TANESCO Longido Mhandisi. Lazaro Lenoi, mara baada ya kuulizwa na RC Makonda kuhusu uwepo wa umeme mdogo katika zahanati hiyo, amesema waliunganisha umeme wa single phase kwakuwa ndivyo mahitaji yao walivyoomba kutoka uongozi wa zahanati hiyo.

Kutokana na maji hayo, RC Makonda alimuhoji tena Mhandisi. Lazoro kuwa kwanini baada ya kupata malalamiko kwanini asingefika katika zahanati hiyo kushughulikia, jambo ambalo Meneja TANESCO amesema hajapokea malalamiko wala changamoto yoyote tangu walipounganisha umeme huo.

RC Makonda aliongeza swali kwa Meneja TANESCO na kumuuliza kwanini hakutumia utaalamu wake kutoa ushauri kwa uongozi wa zahanati hiyo ili kuwavutia umeme wa three phase, jambo ambalo amesema alishamueleza Mwenyekiti wa serikali ya kijiji ilipo zahanati hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji Mhe. Supuk Melita, mara baada ya kuulizwa na RC Makonda kuhusu ushauri huo, amekiri kuwa walipokea ushauri huo.

Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili, RC Makonda ameamua kutoa kiasi cha fedha zaidi ya Tsh 100,000/= kuunganishwa kwa three phase katika zahanati hiyo ndani ya siku tatu.

"... hapa ni zahanati na imetumika fedha kwaajili ya kuhakikisha wananchi wa kijiji hiki wanapatiwa huduma ya afya stahiki.. lazima tuwe sehemu ya kumsadia kazi vizuri Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , kwa kutafsiri kazi yake kwa wananchi wa hali ya chini "

" Umeme uunganishwe hapa wa kutosha kwenye zahanati na kwenye nyumba ya watumishi "





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...