Wanafunzi wa awali wa shule ya msingi Tusiime jijini Dar es Salaam walioonyesha kama marubani na wahudumu wa ndege wakati wa maonyesho ya kutengeneza vitu mbali mbali shuleni hapo







 
Watu wakiangalia shanga zilizotengenezwa  na wanafunzi wa shule ya awali Tusiime Tabata Magengeni

Na Mwandishi Wetu

WAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya awali Tusiime leo wameshangazwa na vipaji vilivyoonyeshwa na wanafunzi hao kwa kumudu kutengeneza vitu mbalimbali na kumudu kuzungumza kingereza fasaha muda wote.


Maonyesho hayo yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopoTabata Sanene jijini Dar es Salaam yamehusisha utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo shanga, chakula cha tamaduni za makabila mbalimbali, vifaa vya usafiri wa anga, kuonyesha tamaduni za kimasai, michoro ya vitu mbalimbali.


Wanafunzi hao pia walionyesha umahiri wa kutengeneza juice za aina mbalimbali hali ambayo iliwavutia wazazi na washiriki wengine wa maonyesho hayo.


Mwanafunzi aliyetia fora zaidi ni Vadim Dmitry ambaye alifanikiwa kuwaeleza wageni kuhusu namna ndege inavyotengenezwa, inavyoweza kuruka na kutua salama kwenye njia yake.


Mwanafunzi huyo alikuwa akitoa maelezo hayo kwa lugha ya kingereza bila kubabaika hali ambayo iliwavutia washiriki wa maonyesho hayo ya leo.


Mkuu wa shule hiyo ya awali, Pamela Mbonanibukya amesema umahiri wa wanafunzi hao haujaja kwa urahisi kwani ni kazi kubwa inayofanywa na walimu wa shule hiyo.


Amesema wamefanikiwa kuwa na walimu mahiri na wanaojituma kwenye kazi zao ambao wamekuwa wakiwaandaa wanafunzi kwaaajili ya kupata ujuzi mbalimbali utakaowasaidia siku za baadae.


Amesema kupitia maonyesho hayo wamekuwa wakivumbua vipaji mbalimbali vya wanafunzi ambavyo kama vitaendelezwa vitawasaidia kuja kuwa watu wa kutegemewa sana kwenye jamii.


“Tusiime hatuna jambo dogo, hapa tumeanza na nakuhakikishia wanafunzi hawa watakuja kufanya mambo makubwa sana zaidi ya haya ambayo umeona leo kwasababu kuna mengi tumeandaa,” alisema mwalimu Pamela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...