Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inashiriki maonesho ya 27 ya Wiki ya Unywaji maziwa Kitaifa jijni Mwanza huku ikiwataka wafugaji kutembelea banda zka benki hiyo kwa ajili ya kupata taarifa za fursa mbali mbvali kwa ajili yao.
Akiongea muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa maonesho hayo, Meneja wa TADB Kanda ya Ziwa Alphonce Makoki alisema benki hiyo inatoa mikopo ya riba nafuu kwa wafugaji na kuwataka wafugaji waliopo kanda ya ziwa na maeneo ya Jirani kuchangamkia fursa.
Alisema TADB ni mdau mkubwa kwenye sekta ya mifugo na inatambua umuhimu wa sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa na kuongeza kuwa benki hiyo inatoa mitamba bora kwa wafugaji ambayo inasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa.
“Kupitia mitamba tunayotoa wafugaji wanaweza kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa lita 8 hadi 10 kufikia lita 20 na kuendelea. Maziwa yanapokuwa mengi yanasaidia viwanda vyetu kuweza kusindika na kuuza zaidi,” alisema.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Afia Sigge akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Bodi ya Maziwa Profesa Zacharia Masanyiwa mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 27 ya Wiki ya mwaziwa ynayoendelea jijini Mwanza.
Akiongea muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa maonesho hayo, Meneja wa TADB Kanda ya Ziwa Alphonce Makoki alisema benki hiyo inatoa mikopo ya riba nafuu kwa wafugaji na kuwataka wafugaji waliopo kanda ya ziwa na maeneo ya Jirani kuchangamkia fursa.
Alisema TADB ni mdau mkubwa kwenye sekta ya mifugo na inatambua umuhimu wa sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa na kuongeza kuwa benki hiyo inatoa mitamba bora kwa wafugaji ambayo inasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa.
“Kupitia mitamba tunayotoa wafugaji wanaweza kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa lita 8 hadi 10 kufikia lita 20 na kuendelea. Maziwa yanapokuwa mengi yanasaidia viwanda vyetu kuweza kusindika na kuuza zaidi,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda (kulia) akimsikiliza kaimu mkurugenzi wa Mipango, Ushauri na Mahusiano ya Taasisi kutoka Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Mkani Waziri alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonesho ya 27 ya Wiki ya mwaziwa ynayoendelea jijini Mwanza. Kati kati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Afia Sigge.
Afisa Mwandamizi Maendeleo ya Biashara wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Godwin Elisa akifafanua jambo kwa mteja aliyetembelea banda la benki hiyo katika Maonesho ya 27 ya Wiki ya mwaziwa ynayoendelea jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...