Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akizungumza na waandishi wa habari ljijini Dar es Salaam eo Mei 24, 2024  baada ya kumalizika kikao cha mwaka kilichowakutanisha wana hisa na Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Ishmael Kasekwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo Mei 24, 2024 baada ya kumalizika kikao cha mwaka kilichowakutanisha wana hisa na Watendaji wa TADB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo Mei 24, 2024 baada ya kumalizika kikao cha mwaka kilichowakutanisha wana hisa na Watendaji wa TADB.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Mei 24, 2024 imetoa gawio la shilingi milioni 850 ikiwa imetokana na faida ya shilingi bilioni 14 ambayo wameipata kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa imetofautiana kwa shilingi bilioni 3 za mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo ilikuwa shilingi bilioni 11.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kikao cha mwaka kilichowakutanisha wanahisa na TADB, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema utendaji bora wa TADB mwaka ujao wa fedha serikali inatarajia kuwaongezea mtaji wa zaidi ya bilioni 100.

Pia ameishukuru Menejimeni ya TADB pamoja na bodi kwa kuendelea kusimamia na kuhakikisha uwekezaji wa serikali unaendelea kuimarika na kuwafikia watu wengi zaidi kupitia huduma amesema Mchechu.

Amesema kuwa TADB ni benki ya kimkakati, huku akieleza kuwa kwa asilimia kubwa kilimo kimeajiri watu wengi na kukuza uchumi wa Taifa kwa Ujumla.

Akizungumzia matumizi ya gawio hilo, Mchechu amesema kuwa serikali itaenda kusaidia utekelezaji wa huduma mbalimbali za kijamii huku akieleza kuwa wataendelea kufanya uwekezaji kama wanahisa katika benki ya TADB ambapo mpaka sasa kuna mtaji wa shilingi bilioni 315.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Ishmael Kusekwa, amehaidi kuendelea kutekeleza majukimu yake katika utendaji pamoja na kutimiza majukumu ya benki kama serikali ilivyokusudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa  TADB, Frank Nyabundege, amesema kuwa benki imeendelea kufanya vizuri na kukua kila mwaka katika utendaji wa kazi.

Pia Nyabundege aametoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa ya kupata mkopo kwa ajili ya kilimo cha mazao, ufugaji pamoja na uvuvi.

Pia amesema kuwa Serikali imekuwa ikitusaidia mtaji  wa benki hiyo kwa mwaka huu imetoa shilingi bilioni 170....." 

Tumeendelea kukua na kuwafikia watanzania wengi hasa wakulima, wafugaji na wavuvi na kufikia malengo kwa asilimia kubwa.” Amesema Nyabundege.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...